Breaking News

Your Ad Spot

Feb 5, 2012

CCM YAFUNIKA MWANZA SHEREHE ZA KILELE CHA MAADHIMISHO YA MIAKA YAKE 35

Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete akiwasili kwenye Ofisi ya CCM mkoa wa Mwanza tayari kwa matembezi ya mshikamano yaliyoanza asubuhi sana. Kulia wanaompokea ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Pius Msekwa, Mlezi wa mkoa wa Mwanza, Spika wa Bunge Anna Makinda na katibu Mkuu wa CCM Wilson Mukama.
 Mweneyekiti akimsalimia Katibu mstaafu wa CCM Philip Mangula. Kulia ni Katibu Mkuu mstaafu wa CCM Yussuf Makamba.
 Kisha akamsalimia Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye
 Wanachama wa CCM wakiwa tayari kwa matembezi kuanzia hapo Ofisi ya CCM mkoa wa Mwanza  hadi viwanja vya Furahisha
 Matembezi yakaanza kiasi cha saa 12 na nusu hivi, Jk akiongoza matembezi hayo na Mama Salma Kikwete  bika kukosa.
 Makatibu wakuu wa CCM astaafu Mzee Makamba na Mzee Mangula wakiwa ka Katibu Mkuu wa sasa wa CCM, Wilson Mukama
 Kijana ambaye amelazimika kupatiwa matibabu India baada ya kumwagiwa tindikali usoni na watu wanaodaiwa kuwa wafuasi wa Chadema, wakati wa uchaguzi mdogo jimbo la Igunga Mussa Tesha (kushoto) akishiriki matembezi hayo. Wapili kushoto ni Nape
 Kina Mama wakipungia mikono msafara wa matembezi hayo ulipopita mtaani kwao
 JK na Mama Salma , wakipunga mkono baada ya kuwasili na matembezi hayo Viwanja vya Furahisha
 Walinzi wa Jadi aka Sungusungu wakiwa kirasmi waliposhiriki matembezi hayo
 JK akiwasalimia wananchi baada ya kuwasili baadaye kwenye Uwanja wa CCM Kirumba kuhitimisha maadhimisho ya miaka 35 ya CCM kwa sherehe zilizofana sana leo
 JK akiwasakimia wanachama wake wa CCM anaoaongoza.
 Wakati JK anaingia pikipiki nazo zilitoa burudani ya aina yake kwa kupiga misele pembezoni mwa uwanja
 Nyomi ya watu ilijaa katika uwanja huo na kuufanya unusurike kushindwa kupumua
 Baada ya JK kuteti paredi motomoto la UVCCM likapita mbele yake ku-msaluti. Hiki ni kikosi cha bendera cha paredi hilo ambalo lilihusisha vijana 400 kutoka wilaya zota za mkoa wa Mwanza
 Hili ndilo paredi kama kamera ya mwana-blogu wetu ilivyonasa moja ya gadi wakionyesha ukakamavu
 JK akipokea saluti kutoka kwa Vijana wa CCM waliopita kwa ukakamavu mbele yake. Wengine pichani ni Mskewa, Mabina na kulia kabisa ni Mzee Mukama
 Kabla ya JK kuwasili zilikuwepo burudani kama hii iliyohanikizwa na msanii Marlow
  Watasha aliokuwa Mwanza nao hawakulaza damu, walihudhuria sherehe hizo kuwaunga mkono wana-CCM
 Nyomi ya wana-CCM na wananchi waliojaaa kwenye Uwanja wa Kirymba wakipata burudani  ya msanii Suma Lee akiimba 'Hakunaga kama CCM"
 Wakati Suma Lee akikamua Nape akampa tafu kwa kusakata kiduku jukwaani
 Hawavumi lakini wamo, Huyu ni Katibu Msaidizi Mkuu Idara ya Itikadi na Uenezi Sixtus Mapunda akiimba kibao kilichomo katika albamu ya 'CCM yangu' ambayo imeipuliwa hivi karibuni
 Mama Salma Kikwete akimtuza minoti, Vicky Kamata baada ya kunogewa na wimbo wa mwanamuziki huyo ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum
Licha  ya watu kufurika Uwanjani, lakini wakati wa kuingia ilikuwa kazi pevu kiasi chake kwa kuwa watu waliingia kupitia milango midogo ili kupekuliwa kwa ajili ya usalama, lakini walikomaa na kuingia mmoja baada aya mwingine hadi uwanja ukafurika pomoni!

1 comment:

  1. How to free xrumer 7.0.10 ?
    Send me URL please!!!
    It is the best program for mass posting on forums! XRumer can break most types of captchas!

    ReplyDelete

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages