Breaking News

Your Ad Spot

Feb 8, 2012

LEMA ADAIWA KUMPIGA MWANDISHI WA HABARI MAHAKAMANI LEO

Godbless Lema
Mbunge wa Arusha kwa tiketi ya CHADEMA Godbles Lema amedaiwa kuzusha tafrani katika chumba cha Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kwa kumpiga mwandishi wa habari wa gazeti la serikali la Habari Leo John Mhala kisa eti anagombea benchi la kukalia!

Habari ambazo mtandao huu umezipata kutoka Arusha zimedai kwamba Lema alimpiga mwandishi huyo wakati watu mbalimbali wakiwemo waandishi wa habari wakisubiri kuanza kusikilizwa kesi ya kupinga matokeo ya ubunge wake.

Kwa mujibu wa habari hizo kwa muda mrefu mbunge huyo alikuwa nje ya mahakama hiyo akizungumza na wafuasi wake wakati mwandishi huyo aliyekua amefuatana na wenzake walifika na kukaa katika moja ya benchi lililokuwepo ndani ya mahakama hiyo.

Baada ya kukaa kwa kipindi kirefu bila kesi kuanza kusikilizwa mwandishi huyo alitoka nje kuzungumza na simu na kisha Lema naye aliingia katika chumba cha mahakama akiwa na mkewe na kwenda moja kwa moja katika benchi hilo ambapo alikuta 'note book' ya mwandishi huyo na kuiweka pembeni na kisha akakaa akimulekeza pia mkewe kukaa sehemu hiyo.

"Lema hakukaa katika sehemu hiyo kwa muda mrefu, aliondoka na kwenda meza jirani kuzungumza na baadhi ya waandishi wa habari ambapo Mhala aliingia kisha akakaa sehmu ile aliyokua amekaa awali", alisema mtonya habari wetu.

Alisema katika hali ya kushangaza Lema aligeuka na kumuona mwandishi huyo amekaa akamwendea na kumvuta kwa nguvu na kumsukuma hadi katika meza ile iliyokua ikitumiwa na waandishi hao kisha akamfuata na kumsuma hadi katika kundi kubwa la wasikilizaji wa kes hiyo.

"Wakati wote huo akimsukuma mwandishi huyo Lema alisikika akizungumza maneno ya kujisifia huku akiwaangalia wasikilizaji hao ambapo wengi walikua wakimwangalia kwa mshangao kutokana na kitendo chake hicho", ilielezwa.

“wewe unakaa katika kiti alichokua amekalia mbunge wewe ni nani kwanza hapa ni kiti cha washitakiwa tuu wewe unakaa hapa ni nani unajilinganisha na mbunge lazima uheshimu mamlaka na nafasi yangu kama mbunge sawa” Lema alidaiwa kumwambia mwandishi huyo wakati akimsulubu.

Mbali na maneno hayo inadaiwa Lema pia alisikika akitamka wazi kuwa aliudhiwa na mwandishi huyo kutokana na habari yake aliyowahi kuiandika katika gazeti lake abayo ilmuhusu yeye na aliyewahi kuwa katibu wake kama mbunge aliyedaiwa kukamatwa na silaha aina ya SMG.

“huyu mbaya sana aliwahi kuandika katika gazeti lake kuwa katibu wa mbunge amekamatwa na silaha ya SMG na kusababisha yule jamaa kukaa jela miezi sita hadi juzi alipoachiwa” amekaririwa Lema akisema.

Kutokana na kitendo hicho wengi wa wasikilizaji wa kesi hiyo waliokuwepo mahakamani hapo walionekana kushangazwa na kitendo kile pamoja na kuhoji kwamba kama mwandishi huyo hakustahili kukaa kwenye nafasi ile mbona Lema amemweka mkewe?

Kutokana na hali hiyo chama cha waandishi wa habari mkoani hapa kupitia kwa katibu wake Elia Mbonea kimesema kimepokea taarifa hizo za kudhalilishwa kwa mwanachama wake na mbunge huyo na kinatarajia kulifanyia kazi tukio hilo baada ya kuhojiana na mwandishi huyo.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages