Breaking News

Your Ad Spot

Mar 21, 2012

MAJIMAREFU AWAKA KUUNGANISHWA NA NASSARI WA CHADEMA KATIKA PICHA ANAYODAI NI FEKI

'Picha hii nilipigwa nikiwa na huyu mbunge mwenzangu, Vicent Nyerere (kulia), lakini huyu wa kushoto (Joshua Nassari) hakuwepo karibu yangu kabisa! Yeye alikuwa mbali akiamrisha vijana wanichome moto tena akiwa na hasira, tofauti na anavyocheka katika picha hii. Huu ni mchezo mchafu wa kuunganisha picha kwenye kompyuta uliofanywa na CHADEMA na kwa makusudi gazeti hili likaichapisha, baada ya kuona kwamba hatua aliyofanya Nassari ya kutaka niuawe jana ni mbaya sana. Nitalishitaki gazeti hili". Analalamika Mbunge wa Korogwe Vijijini Stephen Ngonyani wakati akionyesha picha inayomuonyesha akiwa katika furaha ya hali ya juu yeye, Nyerere na Nassari. Picha hiyo imechapishwa leo ukurasa wa kwanza gazeti la Mwananchi.
Picha yenyewe anayolalamikia Profesa Majimarefu ndiyo hii kama tulivyojaribu kuinakili kutoka gazeti la mwananchi. Mdau hebu itazame kwa makini, je ni halisi au feki,  hasa ukitazama vizuri kwenye kwapa la Nassari lililokutana na Ngonyani? Pia tunamkaribisha mpigapicha wa picha hii, Edwin Mjwahuzi kama hatajali atupe picha 'orijino' ya hii tuliyonakili kwa ajili ya kuthibitisha ukweli.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages