Breaking News

Your Ad Spot

Mar 1, 2012

SHUKRANI

Ndugu John Hans Badi (PICHANI) ambaye ni mmiliki na Mhariri Mkuu wa Daily Mitikasi Blog, anachukua fursa  hii kutoa shukrani za dhati kwa watu wote walioshiriki, kwa namna moja au nyingine katika kumuuguza hadi maziko ya mpendwa Mama yake Mzazi, Esther Nyimbo Badi  aliyefariki dunia siku ya Jumatano Feb. 22, 2012 Majira ya Saa 12:30 jioni katika  Hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam na baadaye kuzikwa Kijijini Ilembula (W) Njombe, Iringa.

Shukrani za pekee ziwaendee Madaktari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili na Aga Khan ambao walikuwa wakipigania ili kuokoa maisha ya mpendwa marehemu Mama yetu bila kuchoka hadi dakika ya mwisho neno la Mungu lilipotimia.

Shukrani pia ziwaendee Familia yote ya Marehemu Dr. Luhangano Joseph Badi ikiongozwa na Dada yetu Mkubwa Mama Blandina Nyoni, shemeji zetu kwa jitihada walizozifanya za kujaribu kuokoa maisha ya Mama yetu.

Pia nawashukuru  Wanahabari, Bloggers na wadau wote ambao kwa namna moja ama nyingine walijumuika nami katika kunifariji na kunitia moyo katika kipindi hiki kigumu, ama kwa njia ya simu, E-mails, ana kwa ana.

Si rahisi kumtaja mtu mmoja mmoja ila shukrani pia ziwaendee Mama Mdogo Eliza, Binamu zetu pamoja  ndugu jamaa na marafiki.

Sina cha kuwalipa zaidi ya kuwaombea kwa Mungu abariki kila jambo mnalolifanya hapa duniani na hakika mmejiwekea thawabu nyingi kwake. Kwa kuwa kila nafsi itaonja mauti, basi hatuna budi kumshukuru Mungu kwa kutimiza ahadi yake na tuseme: Yeye (Mama Esther Nyimbo Badi) ni wa Mwenyezimungu na kwake Mungu sote tutarejea!

Mungu ampumzishe Mama Esther Nyimbo Badi Mahala Pema Peponi – Amen!

1 comment:

  1. magnificent publish, really informative. I’m wondering why the opposite specialists of this sector don’t realize this. You must proceed your writing. I'm certain, you’ve a huge readers’ base already!
    84HLUL3NT3
    vimax vimax
    Vimax Vimax
    vimax vimax
    comprar brasil vimax

    ReplyDelete

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages