Breaking News

Your Ad Spot

Mar 18, 2012

WATU WAZIDI KUICHANGAMKIA CCM KATIKA KAMPENI ZAKE JIMBO LA ARUMERU

 Msanii wa TOT anayekwenda kwa jina la Juakali, akihamasisha watu, baada ya mgombea wa CCM Arumeru Mashariki, Sioi Sumari na Mratibu kampeni za CCM Mwigulu Nchemba (kulia) kupanda jukwaani katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo Kata ya Kikatiti A Town.
 SISI NI CCM DAMU: wanafunzi wa kidato cha pili shule ya sekondari Kikatiti wakishadadia CCM wakati wa mkutano wa kampeni za CCM Kata ya Kikatiti
 Mgombea ubunge wa CCM jimbo la Arumeru Mashariki, Sioi Sumari akiwasalimia wapigakura wake, kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kijiji cha Mikandini jimboni humo. Kulia ni Mratibu wa kampeni za CCM jimboni humo, Mwigulu Nchemba.
 Sioi akikasalimia katoto kwenye mkutano huo
 Wazee wa Kijiji cha Maroroni jimbo la Arumeru Mashariki  wakifuatilia kwa makini hotuba ya mgombea wa CCM wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye kijiji hicho.

 NI CCM TU: Kina mama na kina baba wa kijiji cha Mikandini wakishangilia  kwenye mkutano uliofanyika katika kijiji hicho.
 Wananchi wa Kijiji cha  Maroroni wakiwa wameketi kwenye mawe ili kuweza kupata kwa undani zaidi hotuba ya mgombea wa CCM Sioi Sumari kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika katika kijiji hicho.
Msafara wa mgombea wa CCM ulichanja mbuga katika maeneo ya Kata ya Kikatiti kusaka kura jimboni Arumeru Mashariki

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages