Akatumia fursa hiyo kuelezea uzoefu wa Tanzania katika uboreshaji na uendelezaji wa kilimo endelevu na chenye tija, uhifadhi wa chakula na suala zima la lishe. Tanzania ni kati ya nchi chache katika bara la Afrika ambazo zinazalisha chakula cha kutosha na ziada kuunzwa katika nchi za jirani. Mwishoni mwa mkutano huo wajumbe walitoka na azimio ambalo litawasilishwa kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, ili mapendekezo yaliyomo katika azimio hilo yaweze kuingizwa kwenye Tamko la Pamoja la Mkutano wa Kimataifa wa Maendeleo Endelevu maarufu kama RIO +20. Mkutano huo utafanyika mwezi June mwaka huu huko Rio de Janeiro , Brazil .
Kutoka kushoto ni Katibu wa Waziri, Bw. Joseph Qamara, Mhe. Waziri Terezya Hoviza( Mb) Kaimu Balozi,Bw. Justin Seruhere na Bw. Julius Ningu Mkurugenzi wa Mazingira
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269