.

DK. SLAA AKWAA KISIKI BUSANDA

Apr 20, 2012


Dk. Slaa
NA MWANDISHI WETU,BUSANDA 20/04/2012 
Katibu Mkuu CHADEMA Dk. Wilbroad Slaa, ameshindwa kufanya mkutano wa hadhara katika mji mdogo wa Katoro,wilayani Geita baada ya kukumbana na kisiki cha mgogoro ndani ya chama hicho.

Habari zilizopatikana kutoka jimboni humo zimedai kuwa Katibu huyo alitakiwa kufanya mkutano wa hadhara katika mji huo lakini ilishindikana kwa hofu ya kutokea vurugu.

''Ni kweli jana asubuhi ulikuwa ufanyike mkutano huo wa hadhara hapo mji mdogo wa Katoro ambao ni ngome yetu kubwa, lakini ameshindwa kutokana na mgogoro mkubwa unaokitafuna chama na badala yake amelazimika kuingia katika mkutano wa ndani wa usuluhishi." amesema mtu wa ndani ya Chadema na kuongeza.

''Kwa kweli hali siyo nzuri na Dk. Mwenyewe alijionea hali halisi. Na katika mkutano wa usuluhisho,iliamuliwa ufanyike mkutano mkuu wa Jimbo ambapo viongozi kadhaa wanaotuhumiwa akiwemo Diwani wa Kata ya Katoro, Bwana Gervas Daudi na Mwenyekiti serikali ya kijiji cha Katoro, Bwana Jerry Mazemule, waliohojiwa mbele ya Dk. Slaa."

Mkutano huo mkuu wa jimbo hilo uliofanyika katika mji mdogo wa Katoro,ulimalizika saa 5 usiku, lakini hakuna suluhisho kiupatikana na kutokana na upepo kuwa mbaya Dk. Slaa alilazimika kuahirisha kufanya mkutano wa hadhara jimboni humo.

Kaimu Katibu wa jimbo la Busanda, Paul Ntalima, amekiri Dk. Slaa kushindwa kufanya mkutano huo ingawa hakupenda kutoa maelezo ya kina.

''Ni kweli Dk. Slaa Hatofanya Mkutano wa Hadhara jimbo la Busanda lakini kumbuka mie si msemaji wa chama endapo utahitaji kufahamu sababu zaidi muulize Katibu wa Chadema Mkoa.''Alisema na kisha kukata simu.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ª