Breaking News

Your Ad Spot

Apr 30, 2012

HABARI KAMILI HUKUMU YA KUVULIWA UBUNGE MBUNGE WA SUMBAWANGA MJINI


Sumbawanga
Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga imemvua Ubunge mbunge wa Sumbawanga mjini, Aeshi Hilal wa CCM, baada ya kufuta matokeo ya Uchaguzi uliofanyika Oktoba 2010.
     Mahakama hiyo imeyafuta matokeo baada ya kuridhika kwamba kulikuwa na kukiukwa kwa baadhi ya taratibu za uchaguzi zilizoathiri matokeo ya uchaguzi huo.
    Habari kutoka Sumbawanga zimesema, hukumu hiyo imetolewa na Jaji wa Mahakama hiyo, Bethuel Mmila katika kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi iliyowasilishwa mahakamani na CHADEMA kikilalamikia kukiukwa kwa baadhi ya taratibu za uchaguzi huo hivyo kusababisha matokeo yasiyo ya haki.
     Katika hukumu hiyo iliyochukua saa tatu na Jaji Mmila imeelezwa kuwa katika kusikiliza shauri hilo mahakama imepokea vielelezo na ushahidi ulioweza kuthibitisha kuwa baadhi ya taratibu za uchaguzi zilikiukwa na hivyo kuathiri matokeo ya uchaguzi huo.
 Baada ya matokeo hayo watu wanaodhaniwa kuwa wafuasi wa CHADEMA kama kawaida yao wameonekana wakitamba mitaani na pikipiki huku wengine wakipaza sauti huko huko mitaani.
    Hata hivyo shamra shamra hizo hakuathiri hali ya usalama wa mji wa Sumbawanaga hasa baada ya polisi kuchukua tahadhari kudhibiti uwezekano wa vibaka kutumia fursa hiyo kufanya uporaji na wizi wa mali za watu.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages