.

KATIBU MYEKA WA KATIBU MKUU WA CCM AFARIKI DUNIA

Apr 10, 2012

Marehemu Mwakitabu
Ofisa Mwandamizi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Makao Makuu mjini Dodoma, Gordon Mwakitabu amefariki dunia, leo alfajiri nyumbani kwake mjini Dodoma.


Taarifa iliyotolewa na  Ofisi ya Katibu  Mkuu wa CCM, mjini Dar es Salaam, imesema, hadi Mwakitabu anafariki alikuwa Katibu Myeka wa Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama na alikuwa ametumikia nafasi hiyo kwa miaka 15 tangu enzi za Makatibu wakuu wa CCM  waliostaafu, Philip Mangula na Yussuf Makamba.


Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Mwakitabu atazikwa keshikutwa mjini Dodoma. 

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช