Breaking News

Your Ad Spot

Apr 12, 2012

KUAPISHWA KWA WAJUMBE WA TUME YA MABADILIKO YA KATIBA.


 THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
              press@ikulu.go.tz             

Fax: 255-22-2113425



PRESIDENT’S OFFICE,
      THE STATE HOUSE,
              P.O. BOX 9120,  
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 
 TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, atawaapisha Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Kesho tarehe 13 April, 2012, saa 3 asubuhi katika viwanja vya Ikulu.

Tume itaanza kazi zake rasmi tarehe 1, Mei, 2012 kama ilivyopangwa na kutangazwa awali.

Kwa kuzingatia umuhimu wa shughuli hii, Nawaomba wahariri mtutumie majina ya waandishi waandamizi ambao watafika ikulu mapema saa 2.00 asubuhi kwa ajili ya shughuli hii.

Tunaomba majina hayo ya wawakilishi wa vyombo vyenu yawasilishwe kwetu mara baada ya kupata taarifa hii na mwisho wakupokea majina itakuwa  saa 12.00 jioni ya leo . 

Tunapenda kusisitiza kuwa waandishi watakaoruhusiwa kuhudhuria shughuli hii ni wale tu ambao tutapokea majina yao kutoka kwa wahariri wa vyombo husika.
Tunaomba ushirikiano wenu na karibuni.


Imetolewa na Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi.
Ikulu-Dar-Es-Salaam
12 April, 2012

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages