Breaking News

Your Ad Spot

May 2, 2012

CHADEMA WANGUKIA PUA JIMBO LA SEGEREA, DK. MAHANGA AISHINDA KESI

 Mbunge wa Segerea, Dar es Salaam, Dk. Makongoro Mahanga (mwenye suti)akitoka mahakama kuu kwa raha zake, huku akishangiliwa na waliokuwa na wadau, baada ua kuibuka mshindi katika kesi iliyokuwa inamkabili ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2010 yaliyompa ushindi. Kesi hiyo ilikuwa imefunguliwa Mahakama Kuu na aliyekuwa mgombea mwenzake wa jimbo hilo kwa tiketi ya Chadema Fred Mpendazoe. Zifuatazo ni picha zaidi za tukio hilo
 Dk. Mahanga akiwa amezungukwa na wananchi wakiwenmo wanachama wa CCM, wakati akitoka mahakamanai
 "Nimefurahi Sana. Haki Imetendeka" akasema Dk. Mahanga baada ya kuhojiwa na vyombo vya habari
 Kutokana na wingi wa watu mahakamani, ilibidi Mahanga atokee malngo wa hakimu kwa kusindikizwa na polisi
 Wakati wa hukumu hiyo, Mpendazoe naye alikuwepo, akapata fursa kuzungumza na vyombo vya habari kuhusu matokeo hayo 
 Barabara ya Kivukoni Front, pakawa hapatoshi kwa shamrashamra kumsindikiza Dk. Mahakanga wakati akiondoka mahakamani.
 Kushindwa kubaya! watu wanaojitambulisha kwa alama kuwa ni wafusi wa Chadema wakionyesha alama ya chama hicho kujifariji.
 Kwa raha zake Dk. Mahanga akiwa katika gari lake akaondoka eneo la Mahakama Kuu, Kivukoni.
Gari la Dk. Mahanga la Unaibu Waziri akaondoka nalo baada ya kujihakikishia ubunge wake, maana angevuliwa ubunge angekuwa si Waziri tena hata kabla ya Rais Kitangaza Baraza jipya la Mawaziri kama alivyoahidi kufanya baada ya baadhi ya mawaziri kulikoroga.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages