Breaking News

Your Ad Spot

May 2, 2012

WASAFIRISHA MAZAO KWA PUNDA ARUMERU KUTOKANA NA UBOVU WA MIUNDOMBINU YA BARABARA

Na Rose Jackson, Arusha
KUTOKANA na ubovu wa miundombinu unaoukabili maeneo mbali mbali hapa nchini  wananchi  wa kijiji cha Engorora Kata ya Kisongo wilayani Arumeru wanalazimika kusafirisha mazao kwa kutumia punda

Tatizo hilo linawakumba huku kijiji hicho kikiwa na wazalishaji wakuuu wa malighafi ya Moramu na Kokoto ambazo hutumika katika utengenezajiwa barabara kuu za mjini

Akiongea katika mahojiano maalumu kijijini hapo Mjumbe wa Serikali ya kijiji Bw Hustin Leyani alisema kuwa  hali hiyo inasababishwa na uongozi wa halamshauri ya Arusha kutokana na Mipango thabiti ya kukarabati Miundombinu katika maeneo ya Vijijini

“hii kata ni moja ya kata ambayo inaweza kutumika vema katika kuleta vyakula, na hata mifugo katika minada mbalimbali ambapo kwa sasa hata jinsi ya kuleta na kubeba vyakula hivyo bado ni shida kubwa sana”alisema bw Leyani

 Nae Elisifa Obedi ambae ni mkazi wa kijiji hicho alisema kutokana na tatizo hilo imepelekea wakulima wa zao la Ngwara ambalo ndilo tegemeo la wakulima kushindwa kufikiwa na Manunuzi katika maeneo yao na hivyo kulazimika kuwatumia wanyama mbali mbali kama vile punda kusafirisha hdi katika maeneo ya masoko.

Mwenyekiti wa kijiji hicho Joseph Laizer alikiri kuwepo kwa matatizo na changamoto kubwa sana katika eneo hilo na kudai kuwa mpaka sasa
jitiada  mbalimbali zimeshaweza kutafutwa kwa ajili ya kuweza kutatua 
kero kama hizo ambazo zinachangia kwa kiwango kikubwa sana kushuka kwa uchumi wa kijiji 

Bw Joseph  alisema kuwa ili kuhakikisha kuwa changamoto hizo zinakwisha  tayari wameshaenda ofisi ya mkurugenzi wa halimashuri ya arusha ili kuweza kunusuru wananchi dhidi ya tatizo

Sanjari na hilo  alizitaka halmashauri kuhakikisha kuwa kila mara zinaangalia sekta muhimu hasa za vijijini kwa kuwa vijiji vingi ndivyo vinavyozalisha vyakula lakini bado vinasahulika kwa kiwango kikubwa sana hali ambayo hata ianfanya bidhaa mbalimbali kama vile vyakula kuuzwa kwa bei ndogo sana.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages