Breaking News

Your Ad Spot

May 2, 2012

MABONDIA WAWILI WATANZANIA WATINGA HATUA YA ROBO YA MASHINDANO YA KUFUZU KUELEKEA OLIMPIKI.

NA MDAU WA MASUMBWI
Mabondia wa  timu ya Taifa yaTanzania, Selemani Kidunda wa uzito wa 69 kgs (welter weight) na Emillian Patrick  56 kgs (bantam weight), wamesonga mbele katika mashindano ya kufuzu kuelekea katika kushiriki mashindano ya Olimpiki yatakayofanyika London Uingereza.

Wamefuzu katika mashindano yaliyoanza tarehe 28/4-5/5/2012 mjini Casablanca Morocco,ambako  Mabondia hao walishinda mapambano yao ya awali kwa Kidunda kumshinda mpinzani wake Kab Thiam wa Senegal kwa RSC na Patrick kumshinda Tewodros Tilahun wa Ethiopia.

Taarifa zilizotolewa na mdau maarufu wa masumbwi hapa nchini, 'Superboxing Coach' Rajabu Mhamila zimesema mabondia hao sasa wamefika katika hatua ya robo fainali wakiwa katika jumla ya mabondia nane waliofikia hatua hiyo na huku idadi inayotakiwa kufuzu ikiwa ni mabondia sita kwa kila uzito.

Mabondia hao kesho tarehe 2/5/2012 watapanda ulingoni kwa Emillian Patrick kucheza na Isaac Dogboe  wa Ghana  na Seleman Kidunda atacheza na Mehdi Khalsi wa Morocco .

Endapo watashinda watakuwa wameingia hatua ya nusu fainali na tayari watakuwa wamefikia hatua ya kupata medali ya shaba .

Tanzania ilipeleka jumla ya wachezaji wanne na viongozi wawili wachezaji wawili Victor Njaiti na Abdalah Kassim walitolewa katika hatua za awali. Viongozi walioambatana na timu ni Michael Changarawe na Remmy Ngabo.

Kwa mara ya mwisho Tanzania ilishiriki mashindano ya Olimpiki upande wa ngumi mwaka 1996 mjini Atlanta.

Kwa habari zaidi mpigie mdau kwa namba hii  0713 588818.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages