Breaking News

Your Ad Spot

May 7, 2012

HOLLANDE ASHINDA URAIS UFARANSA


Hollande

Habari zinasema kuwa mgombea urais wa Ufaransa wa chama cha Kisoshalisti, Francois Hollande, amemshinda rais wa sasa, Nicolas Sarkozy, kwa asili-mia-3 hadi 5. 
      Ikiwa matokeo hayo yatathibitishwa, Bwana Hollande atakuwa rais wa kwanza wa kisoshalisti nchini Ufaransa, kwa kipindi cha miaka 17; na atakuwa wa kwanza kumshinda rais aliyetumika kwa muhula mmoja tu, tangu mwaka wa 1981.
      Wasoshalisti wanasema kazi ya mwanzo ni kufanya majadiliano tena, juu ya sera za kiuchumi za Umoja wa Ulaya.
      Punde baada ya kura za awali kuonesha matokeo, Rais Sarkozy alikiri kuwa ameshindwa, na alimpigia simu Bwana Hollande kumtakia heri.
Taarifa zinazohusiana

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages