Rose Jakson- Arumeru
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida mwanamke mmoja a julikanae kwa jina la Chausiku Selemani(48) mkazi wa maji ya chai mkoani hapa yuko katika hali ya sintofahamu baada ya kubeba mimba ya miaka minne ambayo ni ya mtoto wa 17 na hadi sasa hajui siku ya kujifungua , hali ambayo imemfanya kuwaomba watu wenye mapenzi mema kujitokeza kumsaidia ili aweze kufanyiwa upasuaji.
Chausiku aliyasema hayo nyumbani kwake alipokuwa akiongea na mtandao huu, kuhusiana na hali aliyonayo ambayo imemfanya asijue la kufanya huku akiwa anakabiliwa na hali ngumu ya maisha.
Alisema kuwa katika maisha yake uzazi wake umekuwa wa shida kwa kuwa kila anapozaa mtoto ni lazima tumboni kibakie kiumbe cha miezi miwili hali inayompelekea kuzaa kila mwaka hadi kufanya kufikia watoto 16 ambapo kati ya hao watatu walishafariki dunia .
“Mimi mara ya mwisho kujifungua ilikuwa mwaka 2008 ambapo mara tu baada ya kujifungua nilimwambia daktari aniangalie kuna kitu kimebaki tumboni ,alivyoangalia aliniambia ni uvimbe upo hivyo nahitajika laki tatu na nusu ili nifanyiwe upasuaji lakini kutokana na hali niliyokuwa nayo sikupata fedha hizo hali iliyopeleka kiumbe hicho kukua hadi leo hii ni mtoto namsikia kabisa akichezal akini kila nikipimwa haonekani”alisema chausiku
Aliongeza kuwa ilimlazimu aenda katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Kilimanjaro (KCMC) na ndipo madaktari wa kafanikiwa kumkata mirija ya uzazi ili kuthibiti hali hiyo lakini cha kushangaza uvimbe huo uliendelaea kukua hadi leo hii ambapo ameeleza kuwa kukatwa kwa mirija hiyo huenda ndio chanzo cha ujauzito huo ku kaa tumboni kwa miaka minne.
Kupitia hali hii mama huyo amewaomba watu wenye mapenzi mema wa msaidie kwa lolotelile ikiwa ni pamoja na maombi ili kumwezesha kwenda kufanyiwa upasuaji ili aweze kutolewa kiumbe hicho ambapo kimemfanya hata kushindwa kuwahudumia watoto waliopo kwani ni wadogo na kipato cha mume wake hakitoshelezi.
“Hapa kwangu hali ni mbaya sana kwani hata watoto hawana hata sehemu ya kulala na wengine wanasoma shule hawana hata sare za shule hivyo naombeni hata mkinisaidia kwa maombi naamini mungu atanisaidia “aliongeza
Kwa upande wake diwani wa kata ya maji ya chai Loth Nnko alikiri kuwepo kwa tatizo la mama huyo na kusema kuwa yuko tayari kuangalia namna ya kuwasaidia kuwalipia ada za shule kwa wale watoto wa watakaofaulu darasa la saba.
Amesema mama chausiku anahitaji msaada wa hali na mali hivyo amewataka watanzania wenye mapenzi mema na mama huyo kumsaidia ili aweze kufanyiwa upasuaji hospitali ambapo awali ilitakiwa jumla ya shilingi laki tatu na nusu hivyo huenda kiasi hicho huenda kikawa kimeongezeka
Wasamaria wema wanaweza kutuma mchango wao wa m-pesa kupitia nambari ya simu ya mume wake ambaye ni Elidaima Kimoso 0764-65 02 88
Your Ad Spot
May 22, 2012
Home
Unlabelled
MWANAME ATESEKA NA UJAUZITO WA MIAKA MINNE, ARUSHA
MWANAME ATESEKA NA UJAUZITO WA MIAKA MINNE, ARUSHA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
rose bado mgeni katika tasnia ya habari huyo mama waandishi wenzako wanamfahamu ungewauliza ni tapeli
ReplyDelete