.

WATATU WAUAWA KWA TUHUMA ZA UJAMBAZI ARUSHA

May 22, 2012

Na Rose Jackson,Arusha
Watu watatu wanaotuhumiwa kuwa majambazi wameuwawa na wananchi  wenye hasira kali  katika eneo la Ngusero mjini hapa  kwa silaha za jadi mara baada ya majambazi hayo kubainika kuwa wanapanga mbinu mbalimbali za kuvamia  nyumba
      Hayo yalielezwa mjini hapa na  kamanda wa polisi wa mkoa wa Arusha Bw Thobias Andengenye alipokuwa akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake ambapo  alisema kuwa tukio hilo lilitokea alfajiri ya saa kumi za asubui ambapo majambazi hayo yalifika katika eneo hilo huku yakiwa ndani ya gari
      Alisema kuwa mara baaada ya majambazi hayo kufika katika eneo hilo la tukio wakiwa na gari aina ya Corola lenye namba T830 AHU walianza kuzunguka zunguka katika eneo hilo ili kupanga nyumba ambayo wanaingia hali ambayo iliwashitua wananchi
      Alifafanua kuwa mara baada ya wananchi kutilia shaka gari hilo ambalo lilikuwa na majambazi hao waliamua kuwaweka chini ya ulinzi na kukagua gari hilo ambapo walikutana na Silaha za jadi  pamoja na silaha nyingine ambazo ni za kuvunjia  nyumba hali ambayo ilisababisha waweze kupigwa sana na wananchi hao
      “inavyosemekana ni kwamba hawa majambazi walikuwa wameshazunguka san a na gari lao kwa muda mrefu sana na sasa mara baada ya kuhisiwa wananachi waliamua kujichukulia sheria mkononi na kisha kuanza kuwapiga sana hali ambayo ilisababisha Mauti yao hapo hapo”alisema kamanda Andengenye.
      Aliongeza kuwa mara baada ya Jeshi la Polisi kufika katika eneo hilo waliweza kugundua kuwa kati ya majambazi hayo matatu mawili yalikuwa yanatafutwa na jeshi hilo bila mafanikio kwa kuwa walikuwa wanatuhumiwa kwa makosa ya unyanganyi wa kutumia silaha ndani ya maeneo mbalimbali ya Mji wa Arusha
      Pia alisema kuwa majambazi hayo yalifajhamika  kwa majina ya Philipho Naftari,huku jambazi mmoja amejulikana kwa jina la Utani ambalo ni shidaa na mwingine hajajulikana jina lake huku jitiada za kuwatafuta ndugu zake zikiwa zinaendelea.
      Hataivyo kamanda huyo alisema kuwa pamoja na kuwa waliowawa walikuwa ni majambazi lakiniPolisi inatafuta chanzo halisi cha aliyeanzisha kipigo na kusababisha wengine kuwauwa majambazi hayo kwa kuwa wengeweza kusaidiasana  polisi katika upelelezi wao lakini kwa kuwa wameshawauwa hakuna upelelezi  tena
      Wakati huo huo Jeshi la Polisi mkoani Arusha linamshikilia mkazi mmoja wa longido kwa kosa la kumsukuma Rafiki yake na kisha  kudondoka na kupoteza maisha papo hapo katika baa moja iliyojulikana kwa jina laZebra.
        Kamanda Andengenye alisema kuwa tukio hilo lilitokea  May 20 majira ya saa kumi za jioni ambapo mtu mmoja liyefhamika kwa jina la Abuu Msema alifariki dunia mara baada ya kusukumwa na rafiki yake ambaye aliyejulikana kwa majina ya Frank Mmasi  mkazi wa Longido mjini hapa
        Alisema kuwa katika siku hiyo ya tukio  Marehemu akiwa na rafiki yake wakiwa ndani jya baa ya Zebra walikunywa pombe sana linaendelea na upelelezi zaidi kuhusiana na tukio hilo huku mtuhumiwa naye akiendelea kuhojiwa juu ya mauaji hayo na atafikishwa mahakamani upeleezi utakapokamilika.
     lakini marehemu alikataa kuondoka huku rafiki yake akimtraka aondoke hali ambayo ilimfanya amnyanyue kwa nguvu huku akiwa amelewa na badaye alidondoka chini na kufariki dunia papo hapo

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ª