Breaking News

Your Ad Spot

May 4, 2012

SAFARI LAGER YATENGA SH. MILIONI TISA UNUSU KUZAWADIA WASHINDI POOL TABLE VYUO VYA ELIMU YA JUU, MWAKA HUU

Na Mwandishi Wetu
Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo akitangaza udhamini huo leo
Kushoto ni Mwenyekiti wa TAPA Isaac Togocho
Kampuni ya Bia Tanzania kupitia bia yake ya Safari Lager imetenga jumla ya sh. milioni 9.5 kwa ajili ya zawadi katika michuano ya ngazi ya taifa ya mchezo wa Pool table kwa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu.


Hayo yamesemwa leo na Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo wakati wa uzinduzi wa udhamini mpya wa mwaka huu wa mchezo wa pool Table kwa wanafunzi hao,katika ukumbi wa Safari Pub, mjini Dar es Salaam.


Shelukindo alisema, zawadi katika ngazi ya mikoa timu itakayoshinda nafasi ya kwanza  itapata sh. 500,000, ya pili sh. 300,000, mshindi wa tatu sh. 200,000 na sh.100,000 kwa mshindi wa nne na  upnade wa mchezaji mmoja mmoja, mshindi wa kiume atapata sh.150,000 kwa bingwa na wapili atapata sh. 100,000 huku upande wa wanawake mshindi wa kwanza akipata sh. 100,000 na wapili sh. 50,000.


Shelukindo alisema michuano hiyo inayoitwa 'Safari Lager Higher Leaning Pool Championship", mwaka huu itaanza kutimua vumbi Mei 12 kwa kushirikisha wanafunzi waliopo katika vyuo vya mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro, Dodoma, Iringa, Mbeya, Kilimanjaro, Arusha na Mwanza


Katika michuano kama hiyo ya mwaka jana, Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) ndicho kiliibuka mshindi ngazi ya taifa na kujipatia kombe na sh. milioni 2.5.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages