WANANCHI wa kijiji cha Engorora katika kata ya Kisongo Mkoani hapa wanakabiliwa na changamoto ya uhaba wa nyumba bora ambapo kijiji kizima kina watu 3000 wakati nyumba bora zikiwa ni 100 tu.
Hayo yalielezwa kijijini hapo na Mwenyekiti wa kitongoji cha Engorora kati bw Piniel Lengai alipokuwa akizugumza na mtandao huu kuhusiana na changamoto hasa za makazi bora
Bw. Lengai alisema kuwa uhaba wa nyumba bora ambao unaikabili sana kijiji hicho unatokana na uhaba wa Vipato mbalimbali vya uchumi hali ambayon inasababisha kwa kiwango kikubwa sana makazi duni
Katika hatua nyingine alisema kuwa pia kijiji hicho kinakabikliwa na changamoto ya kutokuwepo kwa maghala ya kuhifadhia Chakula na Mazao mbalimbali hali ambayo inafanya mazao mengi kuharibika sana, hasa wakati wa mavuno
Alifafanua kuwa hasara ambazo wanazipata kutokana na uhaba wa maghala ni pamoja na kuchezea chakula kingi bila mipangilio maalumu kwa kuwa asilimia kubwa sana ya wananchi hawana sehemu maalumu ya kuhifadhia chakula hali ambayo inachangia kwa kiwango kikubwa baa la njaa hasa wakati ambao mavuno ni madogo
Mbali na hayo alisema kuwa Serikali inatakliwa kuhakikisha kuwa inawekeza zaidi vijijini kwa kuhakikisha kuwa wanapata huduma zote imara ikiwemo michakato ya elimu mbalimbali kama vile elimu ya masuala ya uchumi,uzazi na hata afya kwa kuwa wengi wa wananchi wanapata adha mbalimbali kwa uhaba wa elimu za kijamii.
Naye Mwenyekiti wa kijiji hicho Bw Joseph John alisema kuwa endapo kama huduma mbalimbali zitaboreshwa kijijini hapo basi ni wazi kuwa kijiji hicho kitaweza kuwa mstari wa mbele sana katika kuleta mabadiliko makubwa sana hasa kwa upande wa Mazao na Mifugo kwa kuwa uwezo mkubwa bado wanao.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269