NA ROSE, ARUSHA
WANAFUNZI wa Chuo cha Uhasibu, Njiro jijini hapa, wamevamiwa usiku na watu wanaoaminika kuwa ni majambazi na kuporwa vitu mbalimbali vvenye thamani ya zaidi ya Milioni 10.
Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Bw Thobias Andengenye amesema tukio hilo lilitokea juzi, musa wa saa 2 usiku katika eneo la chuo hicho.
Kamanda Andenyenye alisema kuwa siku ya tukio katika nyumba inayomilikiwa na Bw Frank Maungo ambayo inatumikia na wanafunzi hao kama bweni la wavulana lilivamiwa na kundi la vijana ambao wanasadikika kuwa ni majambazi
Aliendelea kusema kuwa mara baada ya kuvamia nyumba hiyo ambayo inatumika kama bweni majambazi hayo yalivunja Milango ya Vyumba vitano na kupora vitu mbalimbali ambavyo vilikuwa vinatumiwa na wanafunzi hao katika shuguli mbalimbali za masomo
Alitaja vitu ambavyo vimeorwa na majambazi hao kuwa ni pamoja simu za aina mbalimbali za mikononi,Laptop za aina mbalimbali sita zenye thamani tofauti tofauti,kadi za benki ambazo zilikuwa zinatumiwa na wanafunzi hao,pamoja na Fedha taslimu ambazo zote zinakamilisha idadi ya zaidi ya Milioni kumi.
“ walipoingia ndani waliiba vitu hivi vyote na baada ya hapo watu hao ambao walikuwa wanadhaniwa ni majambazi walitoweka na vitu hivyo bila ya wanafunzi hao na watu wengine kujua kuwa wametokomea wapi”alisema Kamanda Andengenye
Mbali mna hayo alisema kuwa taarifa za awali zinaonesha kuwa majambazi hayo yaliingia katika bweni hilo la wanafunzi wakiwa na silaha za jadi kama vile Mapanga,na Marungu ambapo mara baada ya kufanikiwa kuingia ndani ya Bweni hilo na wakazingira kila chumba na kisha kuwaamuru wanafunzi watoe kila kitu walichonacho
Kamanda Andengenye aliongeza kuwa hata kwa upande wa Jeshi la Polisi umebaini kuwa wanafunzi hao ndani ya siku ya tukio walikuwa wametoka kuangalia mpira wa Fainali ya Kombe la Mabingwa ya Ulaya kati ya Chelsea na Bayern Munich uliomalizika muda wa saa 6;30 usiku na waliporudi wakaingia kulala katika vyumba vyao bila kufunga lango kuu na njia hiyo ikawa ni rahisi sana kwa majambazi hayo kuingia ndani
Awali kamanda huyo alisema kuwa katiika tukio hilo hakuna mtu yeyote ambaye amejuriliwa na bado jeshi hilo linaendelea na uchunguzi ili kuweza kuwabaini Majambazi hayo ambayo yamefanya uhalifu huo
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269