Nahodha wa timu ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha(IFM), Charles Evance, akikabidhiwa Sh.500,000 na Ofisa Utamaduni wa Wilaya ya Kinondoni, Jumanne Mlimi, baada ya timu yake kuibuka mshindi wa kwanza katika mashindano ya Pool Safari Higher Learning yaliyomalizika, jana, jijini Dar es Salaam.
HABARI KAMILI:
CHUO cha usimamizi wa Fedha cha Dar es Salaam(IFM) wametetea ubingwa wao juzi katika mashindano ya Pool Safari Lager Higher Learning yaliyomalizika kwenye Ufukwe wa Coco Beach jijini Dar es Salaam.
IFM waliutwaa ubingwa huo kwa kuwachapa majirani zao chuo cha Elimu ya Biashara(CBE) 4-0,hivyo kujitwalia tena ubingwa kwa mara ya pili kwa Mkoa wa Dar es Salaam na kuibuka na zawadi ya kitita cha Shilingi laki tano
Mshindi wa pili katika mashindano hayo ni CBE ambao walizawadiwa laki tatu,wapili ni Chuo cha Ardhi ambao walipata laki mbili na wanne ni Chuo cha DIT ambao walipata laki moja.
Wachezaji wa singles(mmoja mmoja) wanaume alishinda Peter Patrick kutoka chuo cha IFM alinyakua ubingwa akifuatiwa na Goodhope Mamkwe kutoka IFM pia,wakati upande wa Wanawake bingwa alikuwa Modesta David kutoka IFM akifuatiwa na Lilian Meiri kutoka chuo cha CBE.
VYUO VINANE VYAFUZU KUSHIRIKI FAINALI ZA SAFARI POOL.
Katika hatua nyingine, vyuo vinane vimefaulu kuingia katika fainali za mashindano ya Pool Safari Higher Learning yatakayofanyika Mkoani Iringa May 26 mwaka huu kutoka katika Mikoa minane.
Akizungumza mratibu wa mashindano hayo, Michael Machellah vyuo vilivyofaulu kuingia katika fainali hizo ni Morogoro ni Chuo Kikuu cha Mzumbe, Kilimanjaro ni Chuo cha Ushirika Moshi(MUCCOBS), Dodoma ni St.John,Arusha ni Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), Mwanza ni St.Augustine,Iringa ni Ruaha(RUCO),Mbeya ni Chuo cha Uhasibu(TAA) na Dar es Salaam ni Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM).
Wachezaji wa singles(mmoja mmoja) wanaume na wanawake kila mkoa watawakilishwa na mabingwa wa kila mkoa ambapo Morogoro ni Moyo Hamza kutoka Chuo cha Ardhi na Fotunate Shija kutoka chuo cha SUA,Kilimanjaro ni Alphael Jackson kutoka MUCCOBS na Suche Anastasia kutoka KCMUCO ,Dodoma ni justace Mhando kutoka MIPANGO na Lemi Jackson kutoka U-DOM na Waku ,Arusha ni Vicent Katiyega kutoka chuo kikuu cha Arusha(UOA) na Violeth Silas kutoka IAA ,Iringa ni Said Mohamed kutoka RUCO na Beatrice kutoka RUCO, Mwanza ni Joachim Mushi kutoka CBE na Agnes Mtalika wa chuo cha Bugando,Mbeya ni na Dar es Salaam ni Feter Patrick kutoka chuo cha IFM na Modesta David kutoka IFM.
Your Ad Spot
May 21, 2012
Home
Unlabelled
IFM MABINGWA SAFARI HIGHER LEARNING DAR
IFM MABINGWA SAFARI HIGHER LEARNING DAR
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269