Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa zinatarajiwa kuzinduliwa keshokutwa mjini Mbeya na Waziri Mkuu Mizengo Pinda ,katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine.
Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake na kuongeza kuwa uzinduzi huo utakwenda sambamba na uzinduzi wa Sensa kitaifa kwa mkoa wa Mbeya.
Kandoro alisema Waziri Mkuu Pinda anatarajiwa kuwasili mkoani hapa, kesho ambapo ztapata nafasi ya kutembelea kiwanda kinachomilikiwa na kampuni ya Marmo E Granito Mines, kilichopo eneo la viwanda kata ya Iyunga.
Alisema baada ya uzinduzi wa uwashaji Mwenge wa Uhuru, Waziri Mkuu ataenda kukakua kiwanda cha nyama cha Tanganyika Parkers ambacho tangu kujengwe hakijawahi kuifanya kazi hiyo.
Mei 12, mwaka huu Pinda ataendelea na ziara yake kwa kutembelea kituo cha Utafiti Uyole, Chuo cha Kilimo Uyole pamoja na Kituo cha Mifugo Uyole, ambapo atapata maelezo yote muhimu juu shughuli zinazofanyika huko.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269