Pichani: Naibu Katibu Mkuu akiwa pamoja na mwenyeji wake na waalikwa wengine walioshiriki chakula cha mchana kilichoandaliwa na Balozi Daniel Bodini wa San Marino. kutoka kushoto ni Bw. Parfait Onanga Anyanga, Mkurugenzi katika Ofisi ya Naibu Katibu Mkuu, Balozi wa Mongolia, Bi. Enkhtsetseg Ochir, Balozi wa Nigeria, Bibi. Joy Ogwu, Balozi Bodini, Dkt. Asha- Rose Migiro na Bw. Vijay Nambier aliyekuwa Msimamizi Mkuu wa Ofisi ya Katibu Mkuu na ambaye sasa ameteuliwa kuwa Mwakilishi Maalum wa Ban Ki Moon huko Myanmar
HABARI KAMILI
Balozi wa Jamhuri ya San Marino katika Umoja wa Mataifa, Bw. Daniele Bodini amemuelezea Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dkt. Asha-Rose Migiro kama kiongozi ambaye katika uongozi wake daima aliweka mbele maslahi ya nchi zote bila ya kujali ukubwa au udogo wa nchi.
Balozi Bodini ametao kauli hiyo siku ya jumatano wakati alipomuandalia chakula cha mchana Dkt. Asha-Rose Migiro kumshukuru kwa mchango wake na ushirikiano aliouonyesha wakati wa uongozi wake.
Chakula hicho cha mchana kiliandaliwa katika makazi ya Balozi Bodini na kuwashirikisha pia Balozi wa Nigeria katika Umoja wa Mataifa Bibi Joy Ogwu, na Balozi wa Mongolia Bi. Enkhtsetseg Ochir. Aidha Balozi huyo wa San Marino Akasema yeye binafsi anashukuru kwa kupata nafasi ya kufanyakazi kwa karibu na Naibu Katibu Mkuu katika maeneo mbalimbali yakiwamo utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo ya Milenia, uanzishwaji wa UN -Women, masuala ya Ulinzi na Usalama na System wide Coherence.
Vile vile akasema Migiro amekuwa mfano wa kuigwa na wanawake, wasichana na watoto wa kike ambao wanamchukulia yeye kama kielelezo cha mafanikio ya wanawake na kwamba ameatia moyo wengi. Akabainisha kwamba yako mambo mengi ambayo Migiro ameyafanya wakati wa uongozi wake na kwamba hapana shaka yataendelea kukumbukwa katika Umoja wa Mataifa.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu akamshukuru kwa heshima hiyo na kwa ushirikiano aliompatia katika, pamoja na mambo mengine kutekeleza majukumu aliyokuwa amekabidhiwa ya kumsaidia Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa. Akasema daima ataienzi heshima hiyo na kuwashukuru wale wote ambao wameshirikiana naye kwa karibu katika utekelezaji wa masuala mengi na muhimu kwa maendeleo ya mwanadamu.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269