Breaking News

Your Ad Spot

Jun 10, 2012

BOB MAKANI WA CHADEMA AMEFARIKI DUNIA

Bob Makani
Naibu Gavana wa kwanza wa Benki Kuu ya Tanzania na Katibu Mkuu wa kwanza wa Chadema ambaye pia amewahi kuwa Mwenyekiti wa chama hicho, Bob Makani amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.
     Habari zilizothibitishwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Freeman Mbowe zimesema, Makani alifariki dunia jijini Dar es Salaam, baada ya kuugua kwa muda mrefu.
     Amesema amefariki katika hopsitali alikokuwa amelazwa na baada ya kufariki mwili wake umehamishiwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, jijni Dar es Salaam.
    Kufuatia kifo cha mwasisi wa Chama hicho, Chadema wamekatisha ziara zao za kuimarisha uhai wa chama zilizokuwa zinaendelea mikoa ya kusini mwa Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages