Breaking News

Your Ad Spot

Jun 10, 2012

WAANDISHI WA HABARI WAFUNDWA KUIFAHAMU KATIBA

Na Rose Jackson,Arusha
WAANDISHI wa habari  wametakiwa kutambua kuwa wana wajibu wa kufuatilia na kuifahamu vyema katiba  na mapungufu yaliyomo ili waweze kuielimisha jamii umuhimu wa kushiriki katika mchakato wa kutoa maoni ya  katiba hiyo
      Sanjari na kuhakikisha kuwa wanazifahamu sera za nchi zinazotungwa ili waweze kufichua mapungufu yaliyomo ndani ya sera hizo.
       Hayo yamesemwa na mkurugenzi mtendaji  wa umoja wa vilabu vya waandishi wa habari Tanzania(UTPC) bw Abubakari Karsan alipokuwa akifungua mafunzo ya siku nne ya kwa wanachama  waandishi wa habari wa Arusha press club( APC)  yanayohusiana na ufuatiliaji wa sera na matumizi ya pesa za  umma  yaliyofanyika mjini hapa.
        Alisema kuwa waandishi wa habari wanapaswa kuifahamu katiba  na malengo yake muhimu kwa kuwa wako baadhi ya waandishi hawajui na kutambua umuhimu wake  hali inayowapelekea kushindwa kuelimisha jamii juu ya mchakato mzima wa katiba.
        “nawaombeni sana waandishi muwe mhimili  katika kuielewa kwanza katiba na mkishaielewa  nyie nyie muwe mfano mzuri wa kuigwa kwa kuhakikisha kuwa wananchi wanaielewa katiba vizuri kwa kutumia kalamu yenu”alisema Karsan
        Sambamba na hilo Karsan aliwataka waandishi kuifahamu kikamilifu sera  mbali mbali zinazotungwa ili waweze kuibua mapungufu ambayo hayatekelezwi na baadhi ya watu.
        “sera ziko za aina mbali mbali kama za afya,elimu,maji na nyinginezo hivyo ili kuipa jamii taarifa sahihi ni vema waandishi wakazijua kwanza sera hizo ili ziwasaidie kufichua mapungufu ambayo hayatekelezeki katika sera hizo”aliongeza
        Aidha aliwataka waandishi hao   watakapopata mafunzo hayo hawana budi kufichua maovu ya matumizi mabaya ya fedha za umma katika Halmashauri nyingi nchini huku akitolea mfano Halmashauri ya Kishapu ambayo imekuwa na hati mbaya ya matumizi ya fedha za Serikali
        Kwa upande wake  mwezeshaji wa mafunzo hayo bw  Pantaleon  Shoki alisema mafunzo hayo   yatawasaidia waandishi kuifahamu sera ambapo wao wataweza wakawaelimisha wananchi umuhimu wa sera na kwa namna inavyotumika  ambapo pia wataweza kubaini sera ambazo hazitekelezeki kwa jamii.
        Alisema kuwa  waandishi wa habari wana nafasi ya Kuanzisha midahalo maalum ya kisera kwa ajili  kujadili sera mbalimbali ili wananchi na wadau  waweze kufahamu sera hizo na kama zina mapungufu waweze  kupaza sauti kwa serikali ili iweze kutekeleza sera hizo.
       Aidha bw Shoki aliwasihi wanahabari hao kutumia mafunzo hayo vizuri  katika kuhakikisha kuwa wanafuatilia  bajeti zinazopangwa na kubaini makosa yake ili waweze kuifikishia jamii taarifa zilizo sahihi.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages