Breaking News

Your Ad Spot

Jun 12, 2012

MAMBO YA SHERIA: MBUNGE WA BAHI KUENDELEA KUPETA NA UBUNGE WAKE AKIHUKUMIWA KIFUNGO CHINI NUSU MWAKA JELA


KATIBU wa Bunge Dk. Thomas Kashililah ametoa ufafanuzi kuwa mbunge wa Bahi, Omar Badweli anayetuhumiwa kwa rushwa ataendele kuwa mbunge hata kama atahukumiwa kifungo cha chini ya miezi sita jela.
Dk. Kashililah alisema hayo jana alipozungumza kwa njia ya simu na mwandishi wa gazeti hili kuwa mbunge huyo bado ni mtuhumiwa na pia kwa mujibu wa katiba atakoma kuwa mbunge kama atahukumiwa kifungo cha kuanzia miezi sita jela.
    Amesema hayo baada ya mbunge huyo Badwel kufunguliwa kesi mahakamani ya tuhuma ya kuomba rushwa ya sh. milioni nane toka halmashauri ya wilaya ya Mkuranga, Pwani.
     Dk. Kashililah alitoa mfano wa mbunge wa Mbarali, Modestus Kilufi ambaye hivi karibuni mahakama ilimtia hatiani kwa kosa la kutishia kuua kwa maneno kwa kukusudia na kumuhukumu kwenda jela miezi 10 au kulipa faini ya Sh. 500,000.
     Hata hivyo Kilufi alilipa faini hiyo na kuachiwa huru na mahakama ya Mbeya.
Alisema hata kama Badwel atafungwa kifungo cha chini ya miezi sita kwa mujibu wa katiba ataendelea kuwa mbunge atakapokuwa amemaliza kifungo chake hicho.
    "Kwa sasa Badwel ni mbunge halali kwani hayo aliyonayo ni tuhuma tu na hatuwezi sisi kama Bunge kumuondoa mpaka ithibitishwe na vyombo husika.
    Ubunge wake utakoma tu endapo atafungwa zaidi ya miezi sita na hii ni kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano.
    Kila mtu ana haki mbele ya sheria anaweza akajitetea na akawa huru, sasa kama umeshamfukuza utafanyaje ni lazima tusubiri," alifafanua Dk. Kashililah.
Alisema kumekuwa na kesi nyingi za kupinga matokeo ya uchaguzi katika maeneo mbalimbali lakini bunge huchukua maamuzi pale mahakama inapomaliza hukumu yake.
‘’Ni katiba hiyo hiyo ndiyo inamapa uhuru Badwel kuendelea kuwa mbunge mpaka hapo atakapohukumiwa na ana haki kama wabunge wengine’’ alisema.  
SOURCE: UHURU

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages