Ikiwa ni wiki moja tu tangu Bodi ya Taifa ya Mashindano ya Miss Utalii Tanzania kutangaza , kuigawa mikoa yote ya Tanzania bara na visiwani katika kanda maalumu za Mashindano hayo ya Miss Utalii Tanzania .
Mvutano mkubwa ulijitokeza mingoni mwa wadau wa Mashindano hayo, kwa upande wa kanda za Miss Utalii Tanzania – Kanda ya Ziwa na Miss Utalii Tanzania – Kanda ya Magharibi, ambapo kila upande ulikuwa ukidai kuongezewa mikoa katika kanda yake, huku mkoa wa Kagera wakitaka kuwa kanda ya Ziwa na Mkoa wa Shinyanga wakitaka kuwa kanda ya Magharibi , huku wakitaka mkoa wa Mara upelekwe kanda ya Ziwa sambamba na Mkoa wa Mwanza.
Chanzo cha mvutano huo imebainika ni kugombea nafasi za kuwa wenyeji wa Fainali za Kanda za Mashindano haya, wakati Shinyanga wakiamini kuwa uwepo wao katika kanda moja na Mara na Mwanza
kutawaondolea fulsa ya heshima ya kuwa wenyeji wa Fainali za Miss Utalii Tanzania – Kanda ya Magharibi kama ambavyo Mkoa wa Mara nao wanaamini kuwa kuwepo katika kanda moja na Mikoa ya Kagera na
Shinyanga kutawaomdolea fulsa ya kupewa heshima hiyo kubwa ya kuwa wenyeji wa Fainali za Miss Utalii Tanzania – Kanda ya Magharibi, huku wakitanabaisha kuwa bora wasiwe na Mashindano hayo Mkoani Mara kuliko kuwekwa kanda moja na Mwanza. Inadhaniwa pia kuwa hofu ya mikoa hiyo kuwa kanda moja na mkoa wa Kagera, ni hisia kuwa Kagera inaweza kupendelewa kuwa wenyeji wa Fainali za kanda kwa kuwa waziri wa Maliasili na Utalii ni mmoja wa wabunge wa Mkoa wa Kagera.
Bodi ya Taifa ya Mashindano ya Miss Utalii Tanzania , imekaa tena na kutafakari na kuzingatia maoni ya wadau mbalimbali wa Utalii,Utamaduni na Mashindano haya, ambapo imeridhia kuwa Mgawanyo wa mikoa na kanda za Mashindano haya ya Miss Utalii Tanzania , unakidhi matakwa ya kukuza na kuyafikisha Mashindano haya kuanzia Ngazi za Vijiji,Majimbo, Wilaya, Mikoa, Taifa na Dunia, aidha Mgawanyo huu umezingatia uwepo wa vivutio vya Utalii, Utamaduni katika maeneo husika na pia gharama za uendeshaji na uandaaji wa kiwango cha kimataifa. Mgawanyo huu ,umezingatia kutoa fulsa kwa kila mkoa kujitangaza
kitalii,kitamaduni na kiuwelezaji kitaifa na kimataifa. Mgawanyo pia unazingatia uungaji mkono na utekelezaji wa vitendo wa sera za taifa za Utalii, Utamaduni, Uwekezaji, Mazingira, Afya, Umasikini, Elimu,
Vijana, Wanawake na watoto kupitia Mashindano haya ya Miss Utalii Tanzania.
Mgawanyo huu utasadia pia kutekeleza malengo mahususi ya Mashindano haya ikiwemo kuhamasisha na kukuza Utalii wa ndani, kupigavita mila, tamaduni komgwe na potofu na kumfanya kila mtanzania kuwa balozi wa Utalii na utamaduni wa Tanzania ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Serikali za kukuza na luifanya Tanzania kuwa miongini mwa nchi zinazoongoza kwa pato la Utalii Duniani, na kufanya kila makao makuu ya wilaya ,mikoa na majiji kuwa na mazingira ya kuvutia watalii wa ndani na nje.
Mgawanyo huu hauna mahusiano yoyote ya jusiasa wala kabila kwani asasi ya Miss Tourism Tanzania Organisation siyo ya kisiasa, kikabila wala kidini,ambayo ipo ili kutekeleza, kuhamasisha na kutafsiri kwa vitendo sera za taifa za Serikali za Utalii, Utamaduni, uwekezaji, Mazingira, Afya, Elimu n.k.
Tunafahamu fika kuwa mkakati huu ni pigo na kikwazo kikubwa kwa wasio
yatakia mema Mashindano haya , ukiwemo ule mtandao wa kuchafua,kudhoofisha na kukwamisha jitihada za ustawi wa Mashindanohaya kitaifa na kimataifa. Mgawanyo kamili wa wa kanda na mikoa wa
Mashindano haya ni kama ifuatavyo:
MGAWANYO WA MIKOA NA KANDA ZA MASHINDANO YA
MISS UTALII TANZANIA
Na. KANDA MIKOA
Miss Utalii Tanzania Kanda ya Mashariki Morogoro, Pwani na Tanga Miss Utalii Tanzania Kanda ya Magharibi Kagera, Shinyanga, Kigoma na Mara Miss Utalii Tanzania Kanda ya Ziwa Mwanza, Geita, Tabora na Shimiyu Miss Utalii Tanzania Kanda ya Kaskazini Arusha, Kilimanjaro na Manyara
Miss Utalii Tanzania Kanda ya Kati Dodoma, Singida na Morogoro Miss Utalii Tanzania Kanda ya
Kusini Nyanda za Juu Mbeya, Rukwa na Katavi Miss Utalii Tanzania Kanda ya Kusini Ruvuma, Iringa na Njombe Miss Utalii Tanzania Vyuo Vikuu Kanda ya Kati Dodoma, Tabora, Singida, Miss Utalii Tanzania Vyuo Vikuu Kanda ya Kusini Ruvuma, Iringa na Njombe Miss Utalii Tanzania Vyuo Vikuu
Kanda ya Pwani Dar es Salaam, Zanzibar, Lindi na Mtwara Miss Utalii Tanzania Vyuo Vikuu Kanda ya Magharibi Kagera, Shinyanga, Kigoma na Mara Miss Utalii Tanzania Vyuo Vikuu Kanda ya Kusini Nyanda za Juu Mbeya, Rukwa na Katavi Miss Utalii Tanzania Vyuo Vikuu Kanda ya Kaskazini Arusha, Kilimanjaro na Manyara Miss Utalii Tanzania Vyuo Vikuu Kanda ya Mashariki Morogoro, Pwani na Tanga Miss Utalii Tanzania Vyuo Vikuu Kanda ya Ziwa Mwanza, Geita, Tabora na Shimiyu
Asante,
Miss Utalii Tanzania ni Alama ya Urithi wa Taifa – Utalii ni Maisha,
Utamaduni ni Uhai wa Taifa.
Erasto Gideon Chipungahelo
Rais na Mtendaji Mkuu Miss Tourism Tanzania Organisation
--
Miss Tourism The Symbol Of National Heritage
Your Ad Spot
Jun 12, 2012
Home
Unlabelled
MAMBO YA MISS UTALII TANZANIA
MAMBO YA MISS UTALII TANZANIA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269