Breaking News

Your Ad Spot

Jun 12, 2012

MASHABIKI WA SOKA TANZANIA KUONA EURO 2012 KUPITIA SIMU ZAO

Dar es Salaam 12 june 2012.
Mashabiki wa soka nchini kote sasa wanaweza kufurahia mechi za Euro 2012, kupitia simu zao za mkononi, Baada ya Dstv Mobile na Vodacom Kushirikiana kutoa huduma ya kibiashara iliyosubiliwa kwa muda mrefu kupitia mtandao wake wa  3G.
     Huduma hiyo ya kibiashara imekuwa ikitolewa katika kipindi cha majaribio kwa mwaka mmoja  na sasa itawapa uwezo maelfu ya watanzania kupata huduma hiyo ambayo imekuwa gumzo kusini mwa jangwa la sahara.
     Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom Tanzania, Rene Meza, amesema kuwa hii ni nafasi ya kipekee kwa wateja wa Vodacom kufurahia huduma hiyo.
    “Huu ni ushirikiano Mkubwa kati ya Vodacom Tanzania na Dstv Mobile na tumepanga kuwapatia wateja wetu huduma nzuri, Tunafurahia kuwa katika ushirikiano huu maana itawawezesha wateja sio tu kupata taarifa bali hata kuburudika bila kujali mahali walipo”
     Kupata huduma hii ya Dstv Mobile ukiwa na simu yako inayowezeshwa na mtandao wa  3G unakwenda katika  m.vodacom.co.tz  na kuanza kupata huduma hiyo moja kwa moja na hakuna haja ya kunnunua simu nyingine.
    “Tunayo furaha kuweza kuwapatia wateja wetu uwezo wa kuangalia vituo mbalimbali vya Television ikiwemo TBC 1, na huduma hii itakidhi mahitaji ya kila rika, kwa kuweza kuangalia katuni na kupata taarifa kutoka pande mbalimbali za dunia” alisema Felix Sengo, ambaye ni Mkurugenzi wa Dstv Mobile Africa Mashariki.
     Vituo vya Televisheni ambavyo wateja wanaweza kuviona kupitia simu zao  ni pamoja Televisheni ya Taifa ya Tbc 1,  Africa Magic Swahili ambayo inaonesha filamu za kitanzania, Africa magic kwa filamu za Nigeria, Televisheni  ya michezo ya Super sport Blits, supersport live events 1 na 2, Chanel O na Trace Urban kwa muziki kutoka sehemu mbalimbali duniani, TBN Africa, Cartoon Network na Boomerang kwa ajili yaburudani kwa watoto.
      Mteja anaweza kupata huduma hiyo kwa kuchagua kwa siku shilingi 1500,au  7500 kwa wiki na shilingi 15000 kwa mwezi. Huduma hii inapatikana popote ambapo mtandao wa 3G wa Vodacom Unapatikana.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages