Breaking News

Your Ad Spot

Jun 12, 2012

REDDS MISS TANZANIA KUTIMUA VUMBI JUMAMOSI HII, 327 CLUB, MIKOCHENI, DAR

Lundenga na Victoria wakizungumza na press leo jijini Dar es Salaam

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Redd’s Original leo imetangaza rasmi kudhamini shindano la kumpata mrembo atakewakilisha taifa katika mashindano ya urembo ya Dunia mwaka huu, yanayojulikana kama “Miss World 2012.
    Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino International ambao ndio waandaaji wa mashindano ya urembo hapa nchini, Hashim Lundenga alisema, anajua wadau wengi wa sanaa ya urembo watastuka kuona mabadiliko hayo.
     " Hii inatokana na kubadilika kwa ratiba ya mashindano ya Miss World toka mwezi wa December ilivyokuwa ikifanyika awali na sasa yatakuwa yakifanyika mwezi Julai hivyo kuwa na tofauti kubwa na ratiba ya mashindano yetu ya Redds Miss Tanzania ambayo huanza mwezi Mei na kumalizika Septemba", alisema .
     Alisemaili Tanzania ispoteze nafasi ya kushiriki mwaka huu, Kamati ya Miss Tanzania kwa ridhaa ya Serikali, iliamua kufanya shindano dogo “Mini competition” ambalo litatoa mshindi atakayewakilisha katika mshindano hayo makubwa Duniani.
      Warembo 10 wataingia kambini tarehe 13 hadi tarehe 17 June, na shindano litafanyika siku ya Juma Mosi tarehe 16 June, katika ukumbi mpya wenye hadhi ya kimataifa wa 327 Club, uliopo Mikocheni.
      Kwa mujibu wa Ludenga ,mshindi ataondoka na kitika cha fedha taslim sh. Milioni mbili, na kupatiwa maandalizi yote kwa ajili ya matayarisho ya safari yake kwenda kwenye mashindano ya Miss World 2012 yatakayofanyika Inner Mongolia – China.
      "Kutokana na umuhimu wa kufanya shindano hili tuliwaomba wadhamini wakuu wa Miss Tanzania, kinywaji cha Redds ili watuwezeshe kufanikisha mchakato huu, nao bila kusita wakakubali, hivyo tunawapongeza sana Redds kwa mchango wao mkubwa katika sanaa ya urembo hapa nchini" alisema Lundega.
       Akizungumzia maandalizi ya shindano hilo, meneja wa kinywaji cha Redds, Victoria Kimaro alisema, kwa upande wa Redds, maandalizi yote yapo tayari, na wanatarajia shindano litakuwa lenye mvuto wa aina yake
        Shindano hili litaanza saa Mbili usiku hadi saa Nne na litakuwa kwa waalikwa tu. Tumeandaa burudani za kutosha na tuna uhakika waalikwa watakaokuja kushuhudia mchakato huu wataridhika na maandalizi haya.
        "Mabadiliko haya ya ratiba za Miss World yataathiri ratiba zetu kwa mwaka huu tu, lakini yatakuwa na matunda mazuri kwetu kwa siku za usoni, kwani Redds Miss Tanzania atakaeshinda mwaka huu atapata muda wa kutosha kujiandaa kwa ajili ya mchakato wa mashindano yajayo ya Miss World", alisema Lundega. Shukrani 2 Jane John Blog

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages