Mwenyekiti Jukwaa la Wahariri Absalom Kibanda |
MHARIRI wa gazeti la Rai, Masiaga Matinyi ( 41) na wengine wawili wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi jijini Arusha wakikabiliwa na mashitaka kudaiwa kueomba rushwa ya sh. milioni 1.5 kutoka kwa Andrea Mahamud, mfanyakazi wa Shirika la Umeme nchini (Tanesco) wilayani monduli mkoani hapa.
Akisomewa kesi hiyo na waendesha mashataka, Rehema Mtota na Hamidu Msimbana mbele ya hakimu Yohana Miyombo ilidaiwa kuwa watuhumiwa hao walifanya kosa hilo kati ya Juni 13 na 14 katika eneo la Monduli.
Ilidaiwa katika kutenda kosa hilo walimshawishi, Andrea Mahamud kutoa rushwa kwa kumtishia kwamba nafasi aliyonayo Tanesco haijakidhi vigezo vinavyohitajika.
Aidha mwendesha mashataka aliwataja watuhumiwa wengine waliokuwa wamafuatana na mahariri huyo kuwa ni Mwita Chomete( 32 ambaye ni dereva wake pamoja na Bora Bidiga (36) ambaye ni binti aliyetoka nae Daar es Saalam na kwamba kwa pamoja walifanya kosa hilo kwa pamoja huku wakijua ni kinyume cha sheria.
Katika shitaka la pili ilidaiwa kwamba Juni 14,muda wa saa 10 jioni, Mwita Chomete alipokea kiasi cha sh. 200,000 kwa niaba ya mshitakiwa wa kwanza bw Matinyi kwa madai hayo hayo ya mwajiriwa huyo wa Tanesco kutokuwa na vigezo.
Baada ya watuhumiwa hao kusomewa mashataka hayo hakimu Yohana alitaja masharti ya dhamana kuwa ni lazima mdhamini kila mmoja awe anafanya kazi kwenye kamapuni inayofahamika na lazima asaini hati ya sh. 500,000 na hakukuwa na pingamizi ya dhama.
upelelezi bado unaendelea ambapo wahishtakiwa wawili wamepata dhamana huku kesi hiyo ikihairishwa hadi juni 29 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269