Breaking News

Your Ad Spot

Jun 11, 2012

RAIS KIKWETE AONGOZA KUANGWA BOB MAKANI DAR

 Rais Jakaya Kikwete akiwasili kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, kuongoza shughuli ya kuuaga mwili wa muasisi wa Chadema na Naibu Gavana wa benki kuu wa zamani, Bob Makani, leo. Wanaomkaribisha ni viongozi wa Chadema, Mwenyekiti Freeman Mbowe, Katibu Mkuu Dk. Wilbrod Slaa na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Zitto Kabwe.
 Rais Kikwete akiwa na viongozi wa Chadema, Mbowe, Dk. Slaa na Zitto Kabwe
 Mwenyekiti wa Tume ya Kuratibu Maoni ya Katiba Mpya, Waziri Mkuu Mstaafu, Joseph Warioba, na Waziri Mkuu mstaafu ambaye ni Mjumbe wa Tume hiyo, Dk. Salim Ahmed Salim, wakiwasili kwenye viwanja vya Karimjee.
 Dk. Slaa akimkaribisha Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye alipowasili kwenye msiba huo kwenye viwanja vya Karimjee, Dar es Salaam
 Nape akikubatiana na Dk. Slaa wakati wakimfariji kwa msiba huo
 Nape akimfariji Mwenyekiti wa Chadema, Mbowe kwenye msiba huo. Dk. Wilbrod Slaa.
 Nape akimsalimia mama wa Zitto Kabwe, Hajjat Shida Salum
 Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama akimsalimia  Jaji Mkuu Mstaafu Barnabas Samatta
 Mwenyekiti wa IPP, Reginarl Mengi akisalimiana na Profesa Philemon Sarungi kwenye msiba huo
 Rais Jakaya Kikwete akiwa na Mbowe na Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal wakati wa kupokea mwili wa marehemu Bob Makani kuingizwa kwenye viwanja vya Karimjee, kwa ajili ya kuagwa.
 Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama akitoa neno kabla ya kuagwa mwili wa marehemu Bob Makani
Baadhi ya mawakili wakiwa kwenye shughuli hiyo ya kuaga mwili wa marehemu Bob Makani ambaye naye alikuwa mwanasheria wa siku nyingi. :Picha: Daily Nkoromo Blog

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages