Breaking News

Your Ad Spot

Jun 5, 2012

TASWA KUTANGAZA ZAWADI KESHO

Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) kwa kushirikiana na wadhamini wa Tuzo za Wanamichezo Bora wa Tanzania mwaka 2011, Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), kesho Jumatano Juni 6, 2012 saa tano asubuhi mgahawa wa City Sports Lounge Posta Dar es Salaam watatangaza zawadi za washindi mbalimbali wa tuzo hizo.
   Pia TASWA na Serengeti watatangaza zawadi ya mshindi wa jumla wa tuzo hiyo kwa mwaka 2011, ambapo sherehe zitafanyika Juni 14 mwaka huu ukumbi wa Diamond Jubilee (VIP), Dar es Salaam.
    Pia Alhamisi ya Juni 7, Kamati ya Tuzo itatangaza majina ya wanamichezo watakaowania tuzo hiyo kwa kila chama, hivyo usikose mahali patakuwa hapohapo na muda utakuwa huohuo.
     Naomba mjulishe na mwenzako kuhusiana na mkutano huo na nakukaribisha sana.
Amir Mhando
Katibu Mkuu TASWA/ Katibu Kamati ya Tuzo ya Wanamichezo Bora
   
Reply to all
   
Forward
       

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages