Breaking News

Your Ad Spot

Jul 6, 2012

IFM YATIMIZA MIAKA TANGU KUANZISHWA MWAKA 1972

Na Tiganya Vincent- MAELEZO- Dar es salaam 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Ramadhan Khijja amesema kuwa Serikali itaendelea kukiwezesha Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) ili kiendelea kuzalisha wataalam mbalimbali watakaochangia kuleta maendeleo nchini.
    Khijja ametoa kauli hiyo jana jijini Dar es salaam mara baada ya kuzindua maadhimisho ya miaka 40 tangu Chuo hicho kilipoanzishwa mwaka 1972 kwa lengo la kuzalisha watalaam wa kada mbalimbali.
    Alisema kuwa Chuo hicho kimeendelea kuwa muhimu katika kuwaendeleza vijana na hata watumishi waliopo kazini na hivyo kuboresha kada mbalimbali ikiwemo elimu juu ya masuala ya bima na fedha.
    Hivyo ametoa wito kwa wazazi kuendelea kuwapeleka watoto wao katika Chuo hicho kwa ajili ya kupata utalaam ambazo utawasaidia wao binafsi na Taifa kwa ujumla.
    Khijja alisema katika ya sasa ni vema wazazi wakawapatia watoto wao elimu kwani ndio itakayowakomboa.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages