.

VODACOM KUWAZAWADIA KUZAWADIA WATAKAOTEMBELEA BANDA LAKE SABASABA

Jul 6, 2012

Dar es Salaam, Julai 6, 2012:
Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania itatoa zawadi kwa washiriki mbalimbali watakaotembelea banda lake kwenye maonyesho ya kimataifa ya Dar es Salaam almaarufu kama sabasaba hapo kesho katika kuadhimisha siku ya tarehe 7 ya mwezi wa saba ambayo ni siku maalum iliyoandaliwa na kupewa jina la Vodacom Day katika maonyesho ya mwaka huu.
        Zawadi zitakazo tolewa ni pamoja na kofia, fulana, kalamu za wino pamoja na zawadi nyinginezo nyingi  na siku hiyo itakuwa ni maalum kwa wateja kupata nafasi ya kuzungumza na wafanyakazi wa Vodacom na kubadillishana mawazo.
       Zawadi hizo, Vodacom ilisema, zitakuwa ni mojawapo ya shughuli kadha wa kadha zitakazofanywa na kampuni hiyo inayoshikilia nafasi ya kwanza katika kutoa huduma ya simu za mkononi nchini.
     "Katika banda letu, wateja wataweza kujisajili katika huduma zetu za M-Pesa hapo hapo, kutuma na kupokea fedha kwa njia hiyo na hata kujiunga kuwa wakala wa Vodacom M-pesa, pamoja na kununua simu za ZTE 520 kwa bei nafuu katika ofa inayoendelea ya shilingi elfu kumi na tatu na pia kupata Modem kwa bei nafuu ya shilingi 30,000 na  wanapata MB500 bure kila mwezi kwa kipindi cha miezi mitatu," alisema Kelvin Twissa, Mkuu wa mawasiliano na Masoko wa Vodacom Tanzania.
     Twissa aliyekuwa akizungumza na waandishi wa Habari alikiri kuwa kampuni hiyo inatambua umuhimu wa maonyesho ya saba saba kwa Watanzania, ikiwa ni fursa kwa watu mbalimbali kuangalia na kulinganisha ubora wa bidhaa zinazozalishwa hapa nchini na kwingineko.
   “Maonyesho haya yana umuhimu Mkubwa. Pamoja na hayo, ni nafasi nzuri kwetu sisi Vodacom kupata nafasi ya kukutana na wateja wetu na kubadillishana mawazo ndio maana tukaandaa siku maalum ya kuwapa zawadi watanzania katika maonyesho haya.” Alisema Kelvin.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช