Na Rose Jackson, Arusha, Tanzania
JAMII za wafugaji na wawindaji wa asili wameeleza vipaumbele vyao juu ya mambo wanayopendelea yaingie kwenye katiba mpya yakijikita zaidi katika masuala ya ardhi, fidia na ulinzi kwa jamii za wawindaji wa asili ambao wako hatarini kutoweka
Aidha wanapendekeza katiba mpya iweke usimamizi wa ardhi mikononi mwa taasisi za kiwakilishi au za kidemokrasia tofauti na sasa ambapo usimamizi wa raslimali uko chini ya Rais na vyombo vya serikali kuu.
Hayo yalisemwa na Mratibuwa katiba initiative, (KAI), William Olenasha wakati wa uzinduzi wa chombo hicho kilichoundwa ikiwani utekelezaji wa maazimio ya mkutano mkubwa wa viongozi mbalimbali wa jamii za kifugaji na wawindaji wa asili ulioitishwa na asasi za PINGOs na ALAPA Novemba 2011.
Alieleza kuwa kutokana na mchakato wa katiba kuwa ni fursa ya kutafutia ufumbuzi wa matatizo yanayokabili jamii za kifugaji na wawindaji wa asili waliona ni vema wakaunda KAI yenye jukumu la kutoa elimu na kuwahamasisha watu wa jamii hizo kujitokeza kushiriki mchakato wa katiba mpya ikiwemo kutoa maoni yao
Aidha Olenasha alitaja vipaumbele hivyo vilivyotokana na maoni yaliyotolewa kwenye mikutano mbalimbali iliyoandaliwa na KAI pamoja na NGO’s zaidi ya 30 ambapo wanataka katiba mpya iweke utaratibuwa kutenga maeneo maalum kwa ajili ya ufugaji kama ambavyo kwa sasa yametengwa maeneo maalum kwa ajili ya uhifadhi wa wanyamapori na misitu sanjari na kutambua ufugaji kama shughuli ya kiuchumi.
Aliongeza kuwa KAI imeona ni vema hizo za wafugaji na wawindaji walipendekeza katiba mpya itambue ardhi ya jamii(community lands) tofauti na utaratibu wa sasa unaotambua ardhi za vijiji hivyo haulindi haki za ardhi za jamii zenye watu wachache kama Wahadzabe na Ndorobo ambao kwa sababu ya idadi yao kuwa ndogo hawawezi kulinda haki na maslahi yao katika ardhi pale wanapokuwa na makundimengine kwenye vijijini
Naye mgeni rasmi kwenye hafla hiyo mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba, Deus Kibamba, aliitaka KAI kuhakikisha inawahamasisha wadau wao kushiriki kwenye mchakato wa katiba kikamifu ikiwemo kujitokeza ili waweze kupendekezwa kuunda bunge maalum la katiba ili kuweza kuhakikisha inapatikana katiba inayokidhi matakwa yao na Taifa kwa ujumla.
Mkurugenzi wa PINGO’s Edward Porokwa alisema kuwa jamii za wafungaji na wawindaji wa asili wameachwa nyuma kimaendeleo hivyo wanamahitaji tofauti na yale ya kiujumla ndiyo maana wameamua kuaInisha maeneo maalum kwa ajili yao kabla ya kuingia kuzungumzia maeneo mengine yanayoshirikisha Watanzania kwa ujumla.
Your Ad Spot
Jul 5, 2012
Home
Unlabelled
MAONI YA KATIBA, WAFUGAJI NA WAWINDAJI WA ASILI WATAJA VIPAUMBELE VYAO
MAONI YA KATIBA, WAFUGAJI NA WAWINDAJI WA ASILI WATAJA VIPAUMBELE VYAO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269