Breaking News

Your Ad Spot

Jul 5, 2012

JUMUIA YA WAZAZI CCM YAIPATIA VIFAA VYA SH. MILIONI TANO ZAHANATI YA KIMARA

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ally Iddi akimkabidhi vifaa vya huduma na tiba, Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Kata ya Kimara, Dk. Alphoncina Mbinda katika hafla maalum iliyofanyika jana, kwenye Zahanati hiyo, Kimara, Dar es Salaam. Vifaa hivyo vya sh. milioni 5.1, vimepatikana kutokana na michango ya wanachama na viongozi wa Jumuia ya Wazazi Tanzania. Wengine katika picha ni baadhi ya viongozi wa Jumuia ya Wazazi, Katibu Mkuu Hamis Dadi (kulia) Katibu Wilaya ya Kinondoni, Stanley Mkandawile (wapili kulia), na katikati ya Makamu na Mganga Mfawidhi ni Kaimu Mwenyekiti wa Jumuia hiyo, Dogo Mabrouk.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages