.

MIJIZI YAKOMBA HADI BASTOLA KATIKA OFISI YA DK. CHEGENI, MWANZA

Jul 31, 2012

Dk. Cheni

Habari tulizopata kutoka jijini Mwanza zinasema, Mbunge wa zamani wa Jimbo la Busega wilayani Magu, Dk. Raphael Chegeni, ameibiwa bastola yake usiku wa kuamkia leo.
   Kwa mujibu wa habari kutoka jijini Mwanza, bastola ya Chegeni imeibwa baada ya majizi kuvunja ofisi yake na kwamba mbali na bastola majizi hayo yameondoka na kasha maalum la kuhifadhiwa fedha na laptop. 
  "Vitu vingine vinavyodaiwa kuibwa katika ofisi hiyo binafsi ya Chegeni iliyopo katika jengo la Benki ya Exim, barabara ya Kenyatta jijini Mwanza, ni pamoja na sefu ya fedha", kimesema chanzo chetu cha habari. 
   Ikithibitisha tukio hilo, polisi mkoani Mwanza, imesema wezi wamekomba sh. Milioni 5 za madafu na Dola 13 za Kimarekani zilizokuwa kwenye sefu hiyo.

1 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช