Breaking News

Your Ad Spot

Jul 28, 2012

MKATABA WA KUDHIBITI BIASHARA YA SILAHA DUNIANI WAKWAMA

Ujumbe wa Tanzania  ambazo kwa mwezi mzima umeshiriki kikamilifu  hadi usiku wa manane pale ilipobidi na kuhakikisha kwamba maslahi ya Tanzania katika  majadiliano ya kidiplomasia ya nchi wanachama kuhusu  Mkataba wa Kisheria wa Kudhibiti Bishaara ya  Silaha duniani yalikuwa yamezingatiwa. Hata hivyo mkutano huo ulioanza Julai Mbili na kumalizika Julai 27 umeshindwa kutoa Mkataba kutokana na  wajumbe kutokukubaliana kuhusu baadhi ya vipengere ambavyo wengine walikuwa wanataka viwe sehemu ya mkataba, huku  wengine wakikataa kata kata. Mkataba huo kama ungepatikana  ulitarajiwa kwamba ungeleta matumaini na unafuu kwa  mamilioni ya watu ambao maisha yao kila siku yamo hatarini kutokana na  matumizi mabaya ya silaha.  Inaelezwa kwamba biashara ya silaha duniani inashika nafasi ya pili baada ya biashara ya madawa ya binadamu. Kutoka kushoto  mstari wa mbele ni Bw. Theobald Kazora kutoka Ofisi ya Rais, Brigedia  Jenerali Dkt. Charles  Muzanila kutoka JWTZ ambaye pia alikuwa kiongozi wa ujumbe, Kaimu Balozi, Dkt. Justin Seruhere ambaye pia alikuwa kiongozi wa ujumbe akisaidia na  Brigedia Jenerali Muzanila na  Bw. John Kinuno ambaye ni wakili kutoka Ofisi ya  Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Kutoka kulia mstari wa nyuma ni Bw. Peter Macomara kutoka  Taasisi ya Kiraia, Brigedia Jenerali Venance Mabeyo kutoka  JWTZ na Kamishna Esaka Mugasa kutoka Jeshi la Polisi na Mwambata Jeshi katika Ubalozi wa Kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa, Meja Wilbert Ibuge ambaye hayupo pichani. 
HABARI ZAIDI BOFYA TANZANIA VISION BLOG

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages