.

MKUTANO WAJADILI KUANZISHWA MKATABA WA KISHERIA WA BIASHARA YA SILAHA DUNIANI (ATT) WAFANYIKA MJINI NEW YORK

Jul 10, 2012

Wataalam kutoka Tanzania  ambao kutokana   ukumbi uliotengwa kufanyika mkutano huo kuwa mdogo kuliko idadi ya wahudhuriaji walilazimika kukaa  ukumbi mwingine  ambao umeandaliwa   mahususi  kwaajili ya kufuatili  kwa njia ya  Video  kile kilichokuwa kikijili katika ukumbi mwingine. kutoka kushoto ni  Brigedia Jenerali Venance Mabeyo ( JWTZ),  Kamishna Esaka Mugasa,(Polisi) , Meja Wilbert Ibuge (mwambata Jeshi Ubalozini),  Wakili  John Kinuno kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na  Bw. Theobald Kazora,  kutoka Idara ya Mambo ya Nje ( Ofisi ya Rais)
Brigedia Generali Dkt. Charles Muzanila  kutoka  Jeshi la  Wananchi wa Tanzania ( JWTZ) akifuatilia kwa makini majadiliano yanayoendelea kuhusu kuanzishwa kwa Mkataba wa Kisheria wa Biashara ya Silaha Duniani (ATT) mkutano huu  muhimu   unafanyika  hapa Umoja wa Mataifa. Ukiwa umeingia wiki yake ya pili tayari  mataifa mengi ambayo yamekwisha kuchangia majadiliano hayo, yameelezea misimamo yao ikiwamo ya kutouridhia  Mkataba huo endapo utakuwa na mwelekeo wa kubinya uhuru wa nchi kulinda watu wake na  mipaka yake, au kama utakuwa unaingilia uhuru wa nchi kujiamulia mambo yake.  Baadhi ya mataifa yamekuwa yakisisitiza kwamba mkataba huo lazima pia uzibane nchi zinazozalisha silaha hizo badala ya kulenga tu nchi zinazonunua. vilevile mataifa mengi yamesisitiza uwazi na ukweli katika mchakato mzima wa majadiliano hayo. mkutano huu ni wamwezi  mmoja  HABARI KAMILI INGIA TANZANIA VISION BLOG... BOFYA HAPA

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ª