.

MWANDISHI WA HABARI AFARIKI DUNIA, NI CHRIS MWAMBONDA

Jul 15, 2012

Chri (kushoto) enzi za uhai wake
Habari wadau, naomba kuwajulisha kuwa nimepata taarifa kwamba mwandishi mwenzetu Criss Mwambonda amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.
        Taarifa kutoka kwa ndugu yake aitwaye Obi pamoja na rafiki yake wa karibu Jimmy Chika ni kwamba taratibu za mazishi zinafanywa nyumbani kwao Mbezi, Dar es Salaam.
        Mambo mengine kuhusiana na jambo hili tutajulishana wadau. Ni msiba wa wote na sote njia yetu ni moja.
       Tumuombee Mwenyezi Mungu amuweke mahala pema peponi, marehemu Mwambonda ambaye amefanya kazi vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini" Amesema Katibu wa Chama Cha Waandishi wa Habari za Michezo Nchini (TASWA,) Amiri Mhando.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช