.

POLISI WASTAAFU WAUNDA CHAMA, WAFANYA UCHAGUZI WA VIONGOZI

Jul 29, 2012

NA FRANK GEOFREY, JESHI LA POLISI
Chama cha Askari Wastaafu wa Jeshi la Polisi (TAPOA) kimefanya Uchaguzi wake wa Viongozi katika nyadhifa mbalimbali ambao watakiongoza kufikia malengo yake ambayo nikuwaletea maendeleo wanachama wake.

Viongozi waliochaguliwa katika uchaguzi huo na nyazifa zao kwenye mabano ni pamoja na Hilary Rashid (Mwenyekiti), Mustapha Wangwi(Mwenyekiti Msaidizi),Chai Msugar (Katibu),Fadhili Walele (Katibu Msaidizi), SSP Mstaafu Galimanywa (Mweka Hazina), Moses Lyimo (Mwanasheria wa Chama), Wajumbe wa Kamati ya Utendaji Na Wadhamini wa TAPOA.


Akizungumza mara baada ya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa TAPOA Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Polisi Bw.Hilary Rashid ametoa wito kwa Askari wastaafu wote wa Jeshi la Polisi kujiunga katika Chama hicho kwakuwa kitawasaidia katika kupata maendeleo na kudai stahiki zao.

Amesema hivi sasa ni wakati muafaka kwa wastaafu kujitokeza kwa wingi na kulisaidia Jeshi la Polisi katika kuimarisha dhana ya ulinzi shirikishi na Polisi Jamii ili kupunguza uhalifu hapa nchini.


Kwa upande wake Katibu wa TAPOA Kamishna Msaidizi Mwandamizi Mstaafu wa Polisi , Bw.Chai Msugar alisema umoja huo utawawezesha kukutana mara kwa mara nakubadilishana mawazo bila kusahau kushirikiana katika shughuli mbalimbali kwa hali na mali.

Aidha Bw Msugar alisema lengo la Chama hicho nikuhakikisha kinamfikia kila Mstaafu popote pale alipo ili kuweza kupata wanachama wengi ambao watakiimarisha kwakushirikiana na uongozi wa Jeshi la Polisi.

Naye Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Naibu Kamishna Mstaafu Abbas Mwamasoli alisema changamoto wanayokabilina nayo ni kuhakikisha wanafika kila mkoa na kufungua matawi ili iwe rahisi kuwafikia wanachama wote walioostaafu wakiwa na  vyeo mbalimbali bila ubaguzi wowote.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช