Breaking News

Your Ad Spot

Jul 1, 2012

RAIS KIKWETE AFUNGUKA KUHUSU MGOMO WA MADAKTARI

DAR ES SALAAM, TANZANIA 
Rais Jakaya Kikwete amesema serikali haitawalipa madaktari mishahara ya sh. milioni 3.5 wanayoshinikiza kupata na badala yake imewataka wasiokubali kuendelea na kazi waondoke.
   Katika hotuba yake ya mwisho wa mwezi Juni, aliyoitoa le, Rais Kikwete amesema serikali haina uwezo wa kulipa kiasi hicho kwa kuwa uwezo wake ni mdogo.
    “Kutokana na ukweli huo basi kama kuna daktari anayeona kuwa hawezi kufanya kazi serikalini bila kulipwa mshahara huo, awe huru kuacha kazi na kwenda kwa mwajiri anayeweza kumlipa kiasi hicho.  Nasi tutamtakia kila la heri.  Hana sababu ya kugoma ili ashinikize kulipwa mshahara huo. Asisumbuke, hatalipwa mshahara huo,” alisisitiza. Aliongeza kuwa: “Isitoshe, hana sababu ya kuendelea kuwa na mgogoro na mwajiri ambaye hana uwezo wa kumlipa anachokitaka.  Huna sababu ya kumpa usumbufu mwajiri wa kukuandikia barua ya kujieleza au kukuachisha kazi.”
    Kutokana na msimamo huo wa serikali, alisema mamlaka za ajira zimeanza kuchukua hatua kwa wote wanaoendelea kugoma.  Kusoma hotuba yote ya Rais Kikwete BOFYA HAPA

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages