Breaking News

Your Ad Spot

Aug 11, 2012

KANGOYE: NITAJENGA CCM YENYE UADILIFU KWA WAZEE

NA MWANDISHI WETU
MGOMBEA wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Jackson     Kangoye, amesema dhamira yake kubwa ni kujenga jumuia adilifu na yenye kusimamia sera, itikadi na siasa ndani ya CCM.
Pia, amesema atashirikiana na vijana nchini kote kwa lengo la kujenga moyo wa kujitegemea na kujiunua kiuchumi na kwamba, katika kutekeleza hilo kwa vitendo walishabuni na kuanzisha mchakato wa uanzishwaji wa Benki ya Vijana Tanzania.
Kangoye aliyasema hayo muda mfupi baada ya kurejesha fomu ya kuomba kuteuliwa kuwania nafasi hiyo katika Ofisi za Makao Makuu ya UVCCM mjini Dar es Salaam, ambapo alisema atatumia uzoefu wake akiwa kiongozi wa taasisi ya vijana ya Tanzania Youth Development Agenda (TAYODA), kujenga mshikamano ndani ya UVCCM.
Alisema akiteuliwa kuwania nafasi hiyo na baadaye kushinda, atahakikisha anajenga jumuia yenye maadili mema na inayoheshimu mawazo ya wazee wa CCM na taifa kwa ujumla ili kutoa matumaini na kuona CCM inakuwa kimbilio la pekee katika kuongoza nchi.
"Kuna mambo mengi ambayo tunatakiwa kuyaboresha ndani ya jumuia yetu. Kwa kuzingatia hilo nitazingatia na kuendelea kujifunza mikakati waliyoitumia waasisi wetu na kukifanya chama kuwa na mvuto, ndiyo maana baada ya kuchukua fomu ya kugombea nafasi hii nilienda Butiama na kuweka shada la maua katika makaburi ya waasisi wa Chama, Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Joseph Nyerere aliyekuwa kiongozi wa kwanza wa Tanu Youth League ikiwa ni ishara ya kuwaheshimu na kutambua juhudi zao," alisema Kangoye.
Alipotakiwa kueleza matarajio ya vijana wa CCM kutoka kwake, Kangoye alisema watarajie utumishi bora na unyenyekevu wenye kuwaheshimu vijana wote na kuyafanyia kazi mawazo yao yenye nia ya kujenga nchi yetu.
Alisema matarajio ni kuwa na ubunifu wa mikakati mbalimbali ya kiuchumi kwa kuzingatia uzoefu alioupata ndani ya TAYODA, ambapo msingi wake mkubwa ni kumwandaa kijana kuwa tayari kutumia nguvu zake katika kujiletea maendeleo na ndiyo sababu ya kujinadi kupitia kauli mbiu ya Nguvu ya Kijana ni Mtaji wa Maendeleo.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages