.

MAHAKAMA: PROFESA MAHALU HANA HATIA

Aug 9, 2012

Mahakama ya Hakim Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam, imemwachia huru baada ya kumuona hana hatia, aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Mahalu, kuhusiana na kesi iliyokuwa inamkabili katika mahakama hiyo ya kufuja fedha za umma. Zifuatazo ni baadhi ya picha za tukio hilo.

 Aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Prof. Costa Mahalu akikumbatiana kwa furaha na mdogo wake Vilasi Rama baada Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam leo, kumuachia huru katika kesi ya kuhujumu uchumi iliyokuwa ikimkabili.
 Prof.Costa Mahalu katikati akitoka nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam huku akiongozana na wakili wake, Mabere Marando (kushoto).
  Prof.Costa Mahalu akipeana mkono na ndugu na jamaa waliofika mahakamani hapo wakati wa hukumu.
 Prof.Costa Mahalu akizungumza na waandishi wa habari.
 Aliyekuwa Ofisa utawala katika ubalozi wa Tanzania nchini Italia, Grace Martin akitoka Mahakamani. (Picha zote na Daniel Mwita).

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช