.

MKUU WA WILAYA YA SERENGETI AFARIKI DUNIA

Aug 22, 2012


MKUU wa wilaya ya Serengeti Kepteni mstaafu, James Lyamungu amefariki dunia katika hospitali ya Taifa Mhimbili  Dar es Salaam, baada yakupelekwa  kupata matibabu.

Awali Mkuu huyo aliyekuwa amelazwa katika hospitali ya rufaa ya Bugando mkoa wa Mwanza amefariki dunia baada ya kuhamishiwa katika hospitali ya mhimbili baada ya hali yakekuzidi kubadilika.

Marehemu Lyamungu amefariki dunia leo asubuhi  wakati akipewa matibabu katika hospitali  hiyo ya mhimbili na mwili wake umehifadhiwa .

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Mara John Tuppa amesema  kuwa taarifa za msiba  wa mkuu aliyekuwa  mkuu wa wilaya ya Serengeti amezipokea na kwamba wasemaji wakuu juu ya msiba huo ni Makao Makuu.

“Taarifa za Kifo cha marehemu tumeishazituma makao makuu sisi kama mkoa sio wasemaji kwani sio kila mtu atoe taarfa hizi tusubiri zitatolewa na makao makuu kwa vyombo vya habari”,alisema Tuppa.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ª