Breaking News

Your Ad Spot

Aug 26, 2012

DIWANI KWADELO MKOANI DODOMA, AHAMASISHA MAENDELEO

 Mkazi wa Kijiji cha Makirinyi, Khadija Mussa, akikabidhi  kiroba cha alizeti kwa diwani wa Kata ya Kwadelo, Wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma, Omary Kariati kuchangia ujenzi wa zahanati ya Kijiji hicho, wakati wa harambee ya kutafuta fedha za ujenzi wa zahanati, uliondeshwa na diwani huyo, jana. Jumla ya magunia 17 yenye thamani ya sh. 35,000 kila moja, na sh. milioni 9.2 vilipatikana, ikiwa ni pamoja na sh. milioni 7 zilizochangwa na  Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki
 Diwani wa Kata ya Kwadelo wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma, Alhaj, Omary Kariati akiendesha trekta wakati akiwasili kwenye hafla ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kufufua mradi wa maji katika kata hiyo, jana. Jumla ya sh. milioni 4.5, zikiwemo sh. milioni 3, alizochangia waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis
Kagasheki zilipatikana pamoja na gunia 37 za alizeti yenye thamani ya sh. 35,000 kila moja, zikiwemo kumi zilizochangwa na waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe. Kushoto ni Mwenyekiti wa wakulima wa Kwadelo, Sheikh Khamis Nchallo
 Trekta 64 za wakulima wa Kata ya Kwadelo, Kondoa mkoani Dodoma, ambazo wamezipata kwa jitihada za diwani wa kata hiyo, Omary Kariati kutoka Shirika la Uchumi la Jeshi la Kujenga Taifa- SUMA JKT, zikiwa zimeegeshwa eneo la mkutano ulioitishwa na diwani huyo, kwa ajili ya harambee ya kuchangisha fedha
kwa ajili ya kufufua mradi wa maji wa kata hiyo, jana. Wakulima hao walifika na trekta hizo na kuwa mstari wa mbele kuchangia mradi huo wa maji.  Jumla ya sh. milioni 4.5, zikiwemo sh. milioni 3, alizochangia waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki zilipatikana pamoja na gunia 37 za alizeti yenye thamani ya sh. 35,000 kila moja, zikiwemo kumi zilizochangwa na waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.
 Diwani wa Kata ya Kwadelo wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma, Alhaj, Omary Kariati, akionyesha mtaro anaosema uliochimbwa na Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere wakati wa uhai wake mwaka 1973, kwa ajili ya mradi wa maji katika Kata ya Kwadelo, Wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma, jana. Hata hivyo mradi huo ambao ulikuwa ukihudumia watu 1,200 wakati huo, umekufa miaka 20 iliyopita na sasa diwani huyo anaunganisha nguvu za pamoja za wananchi na serikali ya CCM kuufufua. Kwadelo sasa ina watu 11,800.
 Wananchi wa Kata ya Kwadelo wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma, wakiwa kwenye mkutano wa kuchangisha fedha kwa ajili ya kufufua mradi wa maji, katika kata hiyo, jana. Jumla ya sh. milioni 4.5, zikiwemo sh. milioni 3, alizochangia waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki zilipatikana pamoja na gunia 37 za alizeti yenye thamani ya sh. 35,000 kila moja, zikiwemo kumi zilizochangwa
na waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.
 Wazee wa Kata ya Kwadelo, wakipungua mikono kumuaga Diwani wa Kata
 Msichana katika kijiji cha Kwadelo, Wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma akitumia baiskeli kutafuta maji, katika kijiji cha Makiranya, jana
 Kariati akikaribisha nyumbani kwake waandishi wa habari aliofuatana nao kwenye ziara hiyo ya kuhamasisha maendeleo
 Trekta nyumbani kwa diwani wa Kata ya Kwadelo, Omary Kariati

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages