.

MTOTO AOKOTWA PPF TOWER, DAR , APELEKWA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI

Aug 3, 2012

Mtoto huyu (Pichani) ameokotwa eneo la PPF Tower, Jijini Dar es Salaam, leo saa sita mchana akiwa amejilaza.
      Ameletwa Hospitali ya Taifa Muhimbili na polisi wa Kituo Kikuu cha Polisi.  Mtoto huyu anakadiriwa kuwa na umri wa mwaka mmoja na nusu hivi, kwa hiyo hawezi kuongea. 
     Yeyote anayemfahamu mtoto huyu au wazazi wa mtoto huyu ajitokeze na kutoa taarifa sahihi kwetu kupitia namba yangu 0755 64 86 36 au 0715 64 86 36. 
     Mtoto tunaye Hospitalini, anaendelea kuhudumiwa. Tafadhali ukisima taarifa hii isambaza kwa wengine.

Imetolewa na;
Aminiel Buberwa Aligaesha
Afisa Uhusiano Mwandamizi
Hospitali ya Taifa Muhimbili 

DSC05203.JPG
DSC05204.JPG
DSC05205.JPG

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ª