.

Aug 1, 2012

Mwambene

DAR ES SALAAM, TANZANIA
Mwandishi Mahiri wa habari wa siku nyingi, Asah Andrew Mwambene ameteuliwa kuwa Mkurugenzi mpya wa Idara ya Habari (MAELEZO) chini ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.
  Taarifa iliyotolewa leo na Idara hiyo ya habari- MAELEZO, imesema uteuzi huo ni tangu Julai, Mosi Mwaka huu wa 2012.
   "Bwana Mwambene anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Clement Mshana, ambaye mwaka jana aliteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC)", imeema taarifa hiyo. 
   Mwambene (41) kabla ya uteuzi huu alikuwa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa pia  amewahi kufanya kazi katika Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) akiwa mwakilishi wa Kampuni hiyo, Zanzibar. 
Idara ya Habari (MAELEZO) ndiyo Msemaji Mkuu wa Serikali hapa nchini. Mtayarishaji Mkuu wa Daily Nkoromo Blog na timu nzima tunampongeza bwana Mwambene

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ª