Ubao ukionyesha namna kila nchi ilivyopiga kura wakati Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, lilipokutana siku ya Ijumaa kulipigia kura Azimio liliwasilishwa na Saudi Arabia. Azimio ambalo pamoja na mambo mengine lilikuwa linajaribu kutoa shinikizo kwa utawala wa Syria kuacha matumizi ya silaha dhidi ya wananchi wake, lakini wakati huo huo Azimio hilo kutoonyesha ukali wowote kwa upande wa Upinzani, vikundi vya kigaidi au nchi ambazo zimekuwa zikiwapatia wapinzani silaha. Azimio hili limepitishwa kwa kupigiwa kura ambapo nchi 133 zimeunga mkono, 12 zimepiga kura ya hapana huku 31 zikipiga kura ya kutofungamana na upande wowote. nchi ambazo zimepiga kura ya hapana na zile ambazo hazikufungamana na upande wowote baadhi zimeeleza kwamba zimechukua hatua hiyo kutokana na ukweli kwamba azimio hilo limeegemea zaidi upande mmoja, lakini pia lilikuwa linaingilia masuala ya ndani ya nchi huru jambo ambalo ni kinyume na sheria za kimataifa
Your Ad Spot
Aug 5, 2012
Home
Unlabelled
UMOJA WA MATAIFA WAJARIBU TENA KUIBANA SYRIA
UMOJA WA MATAIFA WAJARIBU TENA KUIBANA SYRIA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269