.

ABAMBWA NA POLISI KWA KUPATIKANA NA SILAHA

Aug 5, 2012

NA LUPOY KUNG'ALO, JESHI LA POLISI, DODOMA, TANZANIA
Jeshi la Polisi mkoani Dodoma linamshikilia mtu mmoja aliyefahamika kwa jina Maboksi Mtewele Mbena  mwenye  umri miaka (64) kwa tuhuma za kupatikana na silaha kinyume cha Sheria.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Bw. Zelothe Stephen alisema tukio hilo lilitokea siku ya ijumaa Agoust 3, mwaka huu saa 09:00 kamili asubuhi katika kijiji cha Gomai Wilaya ya Kongwa mjini humo.

“ Mtuhumiwa ni mkazi wa kijiji cha HembaHemba Wilayani Kongwa,  alikamatwa akiwa na Gobore lisilo na namba  pamoja na Risasi nane za Short  Gun  akiwa njiani kwa miguu akiwa anaelekaea shambani kwake.” alielezea Kamanda Zelothe.

Bw. Zelothe Stephen alieleza kuwa silaha zinazomilikiwa  kiharamu zinaweza kuleta madhara makubwa kwa jamii, zinaweza kutumiwa na wahalifu na kusababisha madhara ya  Mauaji, Unyang’anyi, Ujangili, Wizi wa mifugo miongoni mwa jamii.

“Silaha nu kitu cha hatari sana hivyo ni vyema umiliki wake uwe wa kisheria, sio kila mtu anafaa kumiliki silaha, natoa wito kwa watu wote endapo mtaokota silaha au kugundua maficho ya silaha, tafadhali haraka peleka taarifa katika kituo cha Polisi au katika uongozi wa kijiji/mtaa ili kuepuka madhara niliyosema.” Alisisitiza Kamanda Zelothe.

Kamanda Zelothe Stephen alisema mwananchi wa kawaida ndiye mwathirika wa kwanza wa matukio ya uhalifu, hasa unaohusisha matumizi mabaya ya silaha na kuwataka wanajamii kupitia mkakati wa Polisi Jamii na  Ulinzi Shirikishi  kushiriki katika kudhibiti kuenena kwa silaha haramu kwa kutoa taarifa kwa vyombo vya dola.

Wakati huo huo mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Lucia Thomas, mwenye umri wa miaka (60) mkulima na mkazi wa kijiji cha Image Wilayanii Dodoma amepoteza maisha baada ya kugongwa na gari.

Akizungumzia Tukio hilo Bw. Zelothe Stephen Alisema lilitokea siku ya ijumaa tarehe 3, mwaka huu majira ya saa mbili na nusu asubuhi katika eneo la Cavilan Kata ya Kilimani Manispaa ya Dodoma  kwenye Barabara ya  kuu ya Dodoma / Iringa.

Kamanda Zelothe alilitaja Gari iliyosababisha ajali hiyo kuwa ni  yenye namba za Usajili T. 721 AKT Toyota Hiace iliyokuwa ikiendesha na dereva asiyefahamika lilimgonga mtembea kwa miguu huyo na kusababisha kifo chake.

Aidha alisema Dereva wa gari hiyo alikimbia baada ya kufanya kosa hilo, na Jeshi la Polisi Mkoani humo linaendelea kumsaka ili kufikisha mbele ya sheria kukabiliana na kosa lake.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช