.

MGANGA MKUU KAGERA AKANUSHA MKOA KUWA NA MGONJWA WA EBOLA

Aug 5, 2012

Mganga Mkuu wa mkoa wa Kagera amekanusha kuwepo mtoto ambaye amewekwa  katika uangalizi maalum, katika hospitali ya mkoa huo, baada ya kupatikana na ugonjwa wa Ebola kama ilivyoripotiwa na chombo kimoja cha habari.
 "Waandishi wa habari wasiwe waongo kiasi hiki, ameandika kwamba mtoto amewekwa katika uangalizi maalum na kuwa mganga ambaye hakupenda kutaja jina lake, amesema mtoto huyo anaendelea vizuri. Sasa kama daktari huyo ni mwana taaluma kwa nini afiche jina lake kwa kisingizio kuwa si msemaji? kwa nini asitaje jina lake kiuifanya taarifa yeke iaminike hasa ikizingatiwa kwamba suala lenyewe alilozungumzia ni la ugonjwa wa kutisha?", alihoji daktari huyo wa mkoa wakati akizungumza na kituo cha televisheni cha TBC asubuhi hii katika taarifa ya habari ya kituo hicho.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ª